Liverpool watakutana na wawakilishi wa klabu ya Barcelona katika Jiji la London ili kujadili dili la Luis Suarez ambalo linaaminika kufikia kiasi cha pauni milioni 80.
Mtendaji mkuu wa klabu hiyo ya Anfield,Ian Ayre ataangalia pia uwezekano wa kumpata Alexis Sanchez kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 30.
Barcelona wameonyesha nia kubwa ya kutaka kuipiku Real Madrid katika kupata saini ya nyota huyo wa Uruguay ambaye kwasasa anatumikia adhabu yake ya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi minne.
Klabu ya Arsenal itakamilisha uhamisho wa beki wa kulia,Mathieu Debuchy mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia.
Washika bunduki hao tayari wamefika makubaliano ya ada ya kiasi cha pauni milioni 12 na Newcastle United kwaajili ya kumnyakua Mfaransa huyo.
Klabu ya Tottenham imeandaa kiasi cha pauni milioni 50 kwaajili ya kuwanyakua nyota kadhaa kutoka klabu ya Swansea wakati ambapo Mauricio Pochettino akitazamia kuboresha kikosi chake.
Wachezaji kama Michel Vorm,Ben Davies na Wilfried Bony wamekuwa kwenye orodha ya raia huyo wa Argentina ambaye amekabidhiwa mikoba ndani ya White hart Lane.
Liverpool wataingia kwenye mbio za kumuwania mchezaji anayetakiwa sana na Arsenal,Mario Balotelli kama watamuuza Luis Suarez kwenda Barcelona.
Mshambuliaji huyo wa AC Milan yupo sokoni majira haya ya joto na majogoo wa Anfield watapeleka ofa kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23.
Manchester City wapo katika hatua nzuri ya kukamilisha uhamisho wa beki wa kati wa Mehdi Benatia lakini mpaka klabu hiyo ya Serie A itakapo msajili mbadala wake.
Raia huyo wa Morocco alikuwa mmoja wa nyota walioonyesha uwezo mkubwa sana katika msimu uliopita na kuifanya Roma kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Juventus.
Borussia Monchengladbach wanamtupia macho chipukizi wa Chelsea,Thorgan Hazard ambaye ni mdogo wa Eden ili waweze kumsajili kwa mkopo.
Klabu hiyo ya Stamford Bridge inataka mchezaji huyo apate uzoefu katika kikosi cha kwanza na Schalke,Valencia na Wolfsburg wote wanavutiwa naye.
Uhamisho wa mshambuliaji,Julian Schieber kutoka Borussia Dortmund kwenda Hertha Berlin upo katika hatua za mwisho kufuatia klabu hizo mbili kufika makubaliano ya ada ya uhamisho na mchezaji huyo kwasasa anafanya makubaliano binafsi.
Southampton wapo tayari kumnyakua winga wa FC Twente,Dusan Tadic kwa kiasi cha pauni milioni 9 wakati ambapo Ronald Koeman akitaka kupata mbadala wa Adam Lallana ndani ya St Mary.
Klabu ya Liverpool itarudi kwa Southampton na kutaka kumnasa mchezaji wa tatu kutoka katika klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza huku Brendan Rodgers akimtaka Dejan Lovren ili kuboresha safu yake ya ulinzi na ameandaa kiasi cha pauni milioni 15.
Tottenham watataka kiasi cha pauni milioni 20 kutoka kwa Napoli kama klabu hiyo ya Serie A itaonyesha kumuhitaji kiungo mshambuliaji wa kibrazil,Sandro.
Meneja mpya,Mauricio Pochettino ameonyesha nia ya kutaka kumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aondoke katika klabu hiyo ya London Kaskazini majira haya ya joto.
SUAREZ MBIONI KUIHAMA LIVERPOOL
Reviewed by habari motto
on
1:40 PM
Rating: