TEMBELEA MAJIJI YOTE ILA HAYA HAYAFAII.. NI SHIDDAH HUKO



1. Barquisimeto, Venezuela.
kusafiri sehem mbalimbali za dunia ni namna nzuri zaidi ya kutumia muda wa likizo lakini pia inategemea na sehemu unayotembelea, yafuatayo ni majiji kumi duniani ambayo ni hatari zaidi kutembelea.Ingawa jiji hilo lina makazi zaidi ya milioni moja jiji hilo limekuwa likiandamwa na mauaji karibia kila siku. Jiji hilo lina vyuo vikuu vingi na tasisi zingine za ngazi ya elimu ya juu, richa ya kuwa jiji hilo limewahi kuwa ni sehemu kubwa ya utalii duniani kwa sasa watalii wengi wanaogopa kutembelea jiji hilo.
2. Peshawar, Pakstan
Pakstani ni moja ya nchi hatari sana duniani halikadhalika na jiji hilo la Peshawar, kuna vita kila leo, jiji hilo sio salama na hasa kwa wageni, ingawa jiji hilo lina mahotel nzuri ya wageni mji huo unakabiliwa sana na mashambulizi ya kujitoa mhanga.
3. Sana'a, Yemen
Ni nchi ambayo kisiasa haiko sawasawa , Sana'a ni mji wa biashara wa nchi hiyo na ni mji ambo ni hatari zaidi katika nchi hiyo na duniani. Pamoja na ushirikiano baina ya nchi hiyo na Marekani katika kutunza amani nchini humo lakini bado jiji hilo sio sehemu nzuri ya kutembelea.
4. Acapulco, Mexico.
Acapulco umewahi kuwa moja a jiji maarufu duniani kwa utalii. Mji huo wenye bichi nyingi za kuvutia unakabiliwa na tatizo kubwa la madawa ya kulevya.
5. Distrito, Honduras.
Distrito ni moja ya majiji hatari duniani, jiji hilo linakabiliwa na tatizo kubwa la rushwa na mauaji kutokana na uwepo wa vikundi va kimafia.
6. Maceio, Brazil
Maceio ni mji maarufu wa kibiashara wa steti ya Alagoas, jiji hili hushuhudia mauaji 135 kwa makazi 100,000 kila mwaka. Maceio ni hatari zaidi ata ya Rio de Jeneiro.
7. Mogadishu, Somalia
Jiji la Mogadishu lina ugomvi mkubwa na kikundi cha kigaidi cha Al shabab kwa kipindi cha muda mrefu kitu ambacho kinafanya jiji hilo kuwa sio sehemu salama kwa wananchi wa Somalia na wageni. Serikali ya nchi ya Marekani ilikataa kusaidia nchi hiyo kurudisha amani yake mpaka mwaka 2013 ambapo Marekani ilituma washauri wake wa kijeshi kwenda kusaidia kusuruwisha tatizo hilo.
8. Nairobi, Kenya.
Jiji la Nairobi limekuwa hatari hivi karibuni, watalii wamekua wakikimbia jiji hilo lakini pia limeonekana kuwa hatari zaidi kwa wanawake na kwa sasa  watu hawatembei usiku katika jiji la Nairobi, kikundi cha kigaidi cha Al shabab kimekuwa kikitoa vitisho mara kwa mara katika mji huo.
9. Chihuahua, Mexico
Mexico imekua na listi ya miji mingi sana hatari duniani lakini Chihuahua umeongoza kua hatari zaidi ya yote kutokana na kuwa kama njia ya usafirishaji madawa ya kulevya kuelekea nchini Marekani na Kutoka Marekani kuingia Mexco. Wauzaji wa madawa ya kulevya wameonekana kukontroo jiji hilo, mapigano ya kurushiana risasi mitaani kimekua ni kitu cha kawaida.
10. Cali, Colombia
Majiji mengi katika orodha hii ni kutoka kusini mwa bara la Marekani na ni kwa sababu moja muhimu ya madawa ya kulevya. Cali ni moja ya majiji hayo sio sehemu salama ya kuishi, Colombia haijawahi kuwa na heshima nzuri kimataifa na Karibia itakuwa makazi ya kigaidi miaka michache ijayo. Pamoja na kuwa na vivutio vizuri vya kutembelea majiji mengi ya kusini mwa bara la marekani hakufai kuishi.
TEMBELEA MAJIJI YOTE ILA HAYA HAYAFAII.. NI SHIDDAH HUKO TEMBELEA MAJIJI YOTE ILA HAYA HAYAFAII.. NI SHIDDAH HUKO Reviewed by habari motto on 2:16 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.