Results for "international news"

Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722

10:33 AM
Marekani imerekodi vifo vingi vya ugonjwa wa corona kwa siku huku watu 1,736 wakifariki siku ya Jumanne.

Idadi hiyo inaweka watu waliofariki kutokana na virusi hivyo nchini humo kufikia 12,722 kulingana na data za chuo kikuu cha Johns Hopkins.
Marekani ina wagonjwa 398,000 wa virusi hivyo waliothibitishwa , ikiwa ndio idadi kubwa zaidi duniani .
Wakati hayo yakijiri, Rais wa Marekani Trump ametishia kulikatia fedha shirika la afya Duniani WHO kwa sababu amesema shirika hilo halikutilia maanani kwa namna ilivyopasa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
Trump amelilaumu shirika hilo kwa kuegemea zaidi upande wa China.  Rais huyo wa Marekani amedai kwamba asasi hiyo ya kimataifa ilishirikiana na China katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
Akitoa taarifa juu ya hali ya maambukizi hayo nchini Marekani, Trump alipuuza umuhimu wa taarifa ya mshauri mwandamizi iliyotolewa mapema mwaka huu kutahadharisha juu ya uwezekano wa kulipuka kwa maambukizi hayo. Rais huyo amedai kwamba hakuiona taarifa hiyo.
Badala yake Rais huyo wa Marekani amelishukia shirika la afya duniani WHO na kulitishia kulikatia fedha.Trump amesema asasi hiyo inaegemea sana upande wa China kuhusu mkakati wake wa kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Amedai kwamba Shirika la WHO lilishirikiana na China katika juhudi za nchi hiyo za kupunguza hatari ya mlipuko wa maambukizi hayo.
Rais Trump amesema Shirika hilo limeisifu China ingawa pana sababu ya kuwa na mashaka juu ya idadi rasmi  iliyotolewa na serikali ya China juu ya vifo vilivyotokana na mambukizi ya virusi vya corona
Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722 Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722 Reviewed by habari motto on 10:33 AM Rating: 5

Hii ndiyo Miji bora zaidi kuishi duniani

6:51 AM

Couple in Vienna
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mji mkuu wa Austria, Vienna, umeorodheshwa kuwa mji bora zaidi kwa watu kuishi duniani, na kuchukua nafasi ya mji wa Melbourne wa Australia ambao umeongoza kwa miaka mingi.
Mji wa Harare, Zimbabwe ni miongoni mwa miji ambayo haivutii kwa watu kuishi duniani.
Ni mara ya kwanza kwa jiji la bara Ulaya kuongoza kwenye orodha hiyo ya kila mwaka ambayo huandaliwa na Kitengo cha Uchunguzi cha Jarida la Economist.
Utafiti huo uliorodhesha miji 140 duniani kwa kufuata vigezo mbalimbali vikiwemo uthabiti wa kisiasa na kijamii, visa vya uhalifu, elimu na kupatikana kwa huduma bora ya afya.
Katika utafiti huo, jiji la Manchester ndilo lililoimarika zaidi miongoni mwa miji ya Ulaya ambapo jiji hilo lilipanda hatua 16 hadi nafasi ya 35.
Jiji hilo limo mbele ya London kwa hatua 13, ambalo ndilo pengo kubwa zaidi kwa miji hiyo miwili kwenye orodha hiyo tangu kuanza kuandaliwa kwa orodha hiyo miongo miwili iliyopita.
Jarida la Economist limesema kuimarika kwa Manchester ni kwa sababu ya kuimarishwa kwa usalama.
'Ukakamavu'
Utafiti huo ulikosolewa mwaka jana kwa kuushusha hadhi mji wa Manchester baada ya shambulio la Manchester Arena ambapo watu 22 waliuawa.
Mwaka huu, mhariri wa utafiti huo Roxana Slavcheva amesema jiji la Manchester "limenyesha ukakamavu na kujikwamua kutoka kwa shambulio hilo la kigaidi ambalo lilikuwa imetikisa uthabiti wake.
Bi Slavcheva amesema usalama pia umeimarika katika miji kadha ya Ulaya magharibi.
Kuongoza kwa Vienna ni iashara ya kurejea kwa utulivu kiasi katika maeneo mengi ya Ulaya.
Melbourne ilikuwa awali imeongoza kwa miaka saba mtawaliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMelbourne ilikuwa awali imeongoza kwa miaka saba mtawalia
Kwa mujibu wa utafiti huo, karibu nusu ya miji imeimarika katika mwaka mmoja uliopita.
Melbourne, ambao kwa sasa ni mji wa pili duniani kwenye orodha hiyo, ilikuwa imeongoza kwa miaka saba mfululizo.
Majiji mengine mawili ya Australia pia yamo kwenye orodha ya kumi bora mwaka huu: Sydney na Adelaide.
Upande ule mwingine, mji mkuu wa Syria, Damascus ambao umeathiriwa sana na vita ndio usiopendwa zaidi na watu duniani ukifuatwa na Dhaka nchini Bangladesh na Lagos nchini Nigeria.
Economist wanasema kwamba uhalifu, machafuko, ugaidi na vita vilichangia sana katika kuorodheshwa chini kwa miji iliyoshika mkia.
DamascusHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Miji bora zaidi kuishi duniani 2018
1. Vienna, Austria
2. Melbourne, Australia
3. Osaka, Japan
4. Calgary, Canada
5. Sydney, Australia
6. Vancouver, Canada
7. Tokyo, Japan
8. Toronto, Canada
9. Copenhagen, Denmark
10. Adelaide, Australia

Hii ndiyo Miji bora zaidi kuishi duniani Hii ndiyo Miji bora zaidi kuishi duniani Reviewed by habari motto on 6:51 AM Rating: 5

Vifo na uharibifu mkubwa waripotiwa Ghouta Syria

6:56 AM
Kusitishwa kwa mapigano kungesaidia ugawaji wa misaada ya kibinaadam
Image captionKusitishwa kwa mapigano kungesaidia ugawaji wa misaada ya kibinaadam
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeambiwa kuwa vifo, uharibifu mkubwa na taabu vimeendelea kutokea eneo la Ghouta nchini Syria, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Mkuu wa masuala ya dharura wa umoja wa mataifa Mark Lowcock, amesema vita vinavyoendelea na kuzuiliwa kuingia katika eneo walilopo raia wa kawaida inamaanisha kuwa hakuna msaada utakaoweza kuwafikia.
Image captionMali na maisha ya watu yamekuwa hatarini kwa sababu ya vita
Ameongeza kuwa kusitishwa mapigano kwa saa tano pekee hakutoshi kuwafikia maelfu ya watu waliomo sehemu hiyo.
Wajumbe wa Marekani wameilaumu serikali ya Syria na washirika wake kwa kushindwa kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda.
Mjumbe wa Urusi amesema waasi wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake ndio wakulaumiwa.
NA BBC SWAHILI
Vifo na uharibifu mkubwa waripotiwa Ghouta Syria Vifo na uharibifu mkubwa waripotiwa Ghouta Syria Reviewed by habari motto on 6:56 AM Rating: 5

Ndege Ya Ufaransa Nusura Kupigwa Kombora La Korea Kaskazini

7:02 AM

Ndege moja ya Ufaransa iliokuwa na abiria 330 ilikuwa kilomita 100 pekee na kombora la masafa marefu lililorushwa na Korea Kaskazini maafisa wanasema.

Ndege hiyo ilipita katika eneo ambalo kombora hilo lilinguka dakika 10 baadaye.

Kampuni ya Airfrance inasema kuwa ndege yake haikuwa hatarini lakini imejiweke marufuku ya kusafiri katika anga ya Korea Kaskazini kama tahadhari.
Pentagon inasema kuwa kombora hilo lilipaa katika anga yenye shughuli nyingi.

Maafisa wa Marekani mara kwa mara wamekuwa wakionya kuhusu hatari zinazoletwa na makombora dhidi ya ndege za abiria katika eneo hilo. Kombora la masafa marefu ICBM 

Njia iliotumiwa na ndege hiyo aina ya Boeing 777 inaonyesha kuwa ilikuwa magharibi, mwa Hokkaido, kaskazini mwa taifa la Japan , wakati bora hilo la Korea Kaskazini lilikuwa hewani.

Japan na Marekani inakadiria kwamba kombora hilo lilianguaka kati ya kilomita 100na 150 karibu na ndege hiyo.

"Kombora hilo liliruka katika anga na kuanguka nchini Japan, eneo ambalo hutumika na vyombo vya kibiashara na vile vya uvuvi , msemaji wa Pentagon Jeff Davis alisema


Credit kwa 

Juma Mtanda wa jumamtanda.blogspot.com

Ndege Ya Ufaransa Nusura Kupigwa Kombora La Korea Kaskazini Ndege Ya Ufaransa Nusura Kupigwa Kombora La Korea Kaskazini Reviewed by habari motto on 7:02 AM Rating: 5

Ijue Ligi Pekee Anayoshabikia Raisi Kim Jong-UN

6:36 AM
Image result for Kim Jong-UN

Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-UN amejibainisha kuwa ni shabiki mkubwa wa Ligi Kuu Italia ‘Serie A’.

Hayo yalibainika muda mfupi baada ya kinda wa miaka 18 Kwang-Song Han kufunga bao kwenye klabu yake ya Cagliari nchini Italia hivi karibuni.

Seneta wa Italia, Antonio Razzi hivi karibuni alipokutana na wawakilishi wa nchi za bara Asia, alielezwa kwamba siyo tu Rais Kim amekuwa akifuatilia maendeleo ya mshambuliajia Kwang-Son, pia ni shabiki mkubwa wa ligi hiyo kwa ujumla.

Rais huyo wa Korea yeye ni shabiki mkubwa wa timu za Italia na mara kwa mara hufuatilia mechi za timu hizo zinapocheza.

Kiongozi huyo anayeonekana kama dikteta, ilielezwa kwamba amekuwa akifuatilia kwa karibu ligi ya Seria A na maendeleo ya mchezaji wa nchi yake, Kwang-Son.

Pia amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara hilo kufunga bao kwenye Ligi ya Seria A.

Klabu ya Cagliari ilimsajili mchezaji huyo tangu Februari mwaka huu na mkataba wake utamalizika 2022.

Mchezaji mwingine wa Korea Kaskazini alisajiliwa klabu ya Fiorentina mwaka jana na amekuwa akicheza kwenye timu ya vijana kabla ya kutemwa mwishoni mwa mwaka 2016.
Ijue Ligi Pekee Anayoshabikia Raisi Kim Jong-UN Ijue Ligi Pekee Anayoshabikia Raisi Kim Jong-UN Reviewed by habari motto on 6:36 AM Rating: 5

Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi

2:17 PM

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
Image captionMkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ana fursa nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu kwa mara ya kwanza tangu washinde taji hilo bila kushindwa mwaka 2004.
Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa klabu hiyo,Wenger mwenye umri wa miaka 67,alisema kuwa mshindi wa taji la ligi kuu atakuwa na kati ya pointi 82 na 86 mwaka huu.
Alisema: Hii leo tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania taji la ligi ya Uingereza ikilinganishwa na miaka mitano au sita iliopita.
Ninaamini tuna timu nzuri katika ligi yenye ushindani mkubwa.
Arsenal ni wa pili katika jedwali la ligi,ikiwa ni mojwapo ya timu tatu zenye pointi 20 na wako katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao.
Wenger anasema kuwa anafikiri kwamba anahitaji pointi 62 kutoka kwa mechi 29 zilizosalia kushinda taji .
Leicester ndio mabingwa wa taji hilo msimu uliopita.
''Baada ya mechi 9 ,tuna pointi 20,ikimaanisha kwamba ubingwa huo utaamuliwa na kati ya pointi 82 na 86'',alisema.

na BBC SWAHILI
Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi Reviewed by habari motto on 2:17 PM Rating: 5

Hii Ndiyo Sababu Ya Sumsung Galaxy Note 7 kurudisha gharama Kwa Wateja

1:57 PM
Kampuni ya Sumsung Afrika Mashariki (SEEA) imetangaza kuwabadilishia simu au kuwarudishia gharama zao wateja wote walionunua simu za Samsung Galaxy Note 7 popote duniani.
Hatua hiyo imefuata baada ya kubainika kwamba simu hizo ni hatari kwa sababu betri zake zinalipuka. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga marufuku uingizaji wa simu hizo nchini kwa sababu za kiusalama.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari, watu walionunua simu hizo watabadilishiwa na kupewa simu ya Galaxy S7 au Galaxy S7 Edge au Galaxy Note 5 na watarudishiwa gharama za ziada.
Mbali na kuwabadilishia simu, kampuni hiyo imefafanua kwamba wateja wanaotaka kupewa fedha taslimu watarudishiwa fedha kamili walizonunulia Samsung Galaxy Note 7 kama wana uthibitisho wa risiti.
Hii Ndiyo Sababu Ya Sumsung Galaxy Note 7 kurudisha gharama Kwa Wateja Hii Ndiyo Sababu Ya Sumsung Galaxy Note 7 kurudisha gharama Kwa Wateja Reviewed by habari motto on 1:57 PM Rating: 5

Justin Bieber ashuka jukwaani kwa hasira

1:51 PM
Staa wa muziki wa RnB na Pop, Justin Bieber haishiwi visa. Wakati wa tamasha Jumapili mjini Manchester, Uingereza aliondoka jukwaani na kutupa mic chini baada ya kuwataka mashabiki kutopiga kelele wakati akiimba.
rs_1024x759-161024092720-1024-justin-bieber-manchester
E-News iliripoti kuwa Justin aliawaonya mara ya kwanza mashabiki wasipige kelele wakati anaongea nao lakini hawakusikia. “Nashukuru sana kwa upendo wenu mnaouonyesha kwangu, hizi kelele tafadhali naomba ziachwe, ninashukuru tena lakini sidhani kama ni lazima kwenu kushangilia wakati naongea kwasababu najisikia kama nataka kuunganishwa na ninyi,” Justin aliwasihi mashabiki ambao hata hivyo hawakumsikiliza.
Lakini baadaye Bieber mwenye miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira. “Nahisi kwamba nataka wasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho mnajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana,” alisema.
Justin Bieber ashuka jukwaani kwa hasira Justin Bieber ashuka jukwaani kwa hasira Reviewed by habari motto on 1:51 PM Rating: 5

Msimamo wa Diamond Na WCB

1:51 PM

Diamond amedai kuna wasanii wengi wa kimataifa Afrika na nje ya Afrika wametaka kujiunga na WCB lakini amewakatalia kwa kuwa anatka kukuza wa nyumbani kwanza
Pia amesema sasa hivi hawachukui wasanii wengine wachanga mpaka Ray vanny na harmonize wakue vizuri
Msikilize Hapa:

























































Msimamo wa Diamond Na WCB Msimamo wa Diamond Na WCB Reviewed by habari motto on 1:51 PM Rating: 5

Jumba la Adolf Hitler sasa kutobomolewa

6:05 AM
hitler-house




























Serikali ya Austria imesitisha mpango wake wa kutaka kubomoa nyumba ambazo Adolf Hitler alizaliwa,baada ya jopo la wataalam kusema kuwa halikuwa pendekezo lao.
Waziri wa maswala ya ndani ,Wolfgang Sobotka alitangaza jana kwamba jengo jipya litajengwa mahala hapo.
Lakini katika taarifa yake siku ya Jumanne, sasa ameunga mkono pendekezo hilo la wataalam kwamba kulibadilisha jumba hilo na kulifanya kuwa la serikali ama kitu chochote kinachokaribia hilo kutaathiri kumbukumbu zake.
Limekuwa jumba la kuhiji la watu wa Nazi.
Wataalam hao wamesema kuwa kubomolewa kwa jengo hilo kutaharibu kumbukumbu za watu wa Nazi.
Jumba la Adolf Hitler sasa kutobomolewa Jumba la Adolf Hitler sasa kutobomolewa Reviewed by habari motto on 6:05 AM Rating: 5

Siri Ya Harmonize Kushinda Tuzo AFRIMMA

5:20 AM


Tuzo za AFRIMMA ambazo hutolewa kila mwaka kwa Waafrika mbalimbali waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali hasa za burudani, zimetolewa Dallas Texas Marekani leo ambapo kwenye list yote Watanzania walioshinda ni watatu.

Watanzania walioshinda ni Dj D Ommy wa CloudsFM kupitia show mbalimbali ikiwemoXXL na AMPLIFAYA ambapo ameshinda tuzo ya Dj bora Afrika, mwimbaji Harmonize akishinda tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika 2016 huku Diamond Platnumzakishinda ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.

Sasa miongoni waliotoa pongezi kwa Harmonize ni Diamond Platnumza ambae kupitia instagram alipost picha na kuyaandika haya; hii picha inanikumbusha mwaka jana ulipokuja nipokea airport kutokea@afrimma …ukaniuliza “hivi ipo siku nami nitachaguliwa tunzo yoyote ya kimataifa”….nikakwambia “Ukifanya kazi kwa bidii’


‘Ukimuheshimu kila mtu, ukamuamini na kumuomba Mwenyez Mungu basi Mollah atakufungulia ndoto zako….na leo hii kweli Tunafurahia Ushaindi wako wa Msanii Bora Chipkizi Africa….. Hongera sana@harmonize_tzna shukran sana sana kwa Mashabiki zetu pendwa kwa kura na @Afrimmakwa kuendelea
Siri Ya Harmonize Kushinda Tuzo AFRIMMA Siri Ya Harmonize Kushinda Tuzo AFRIMMA Reviewed by habari motto on 5:20 AM Rating: 5

Jeshi la Iraq laanza operesheni kuikomboa Mosul

5:12 AM
Wanajeshi wa Iraq, wakijiandaa na mapambano
Waziri Mkuu wa Iraq Haider Al Abadi amesema operesheni za kijeshi zimeanza kuurejesha mji wa Mosul, ambao ni wa pili kwa ukubwa.
Mji huo kwa sasa unashikiliwa na wapiganaji wa Islamic State.
Tangazo hilo limetolewa usiku wa manane kupitia Televisheni ya nchi hiyo.
Mji wa Mosul ulishikiliwa na wapiganaji hao wa IS, wakati wa mapigano makali na kushuhudiwa eneo kubwa magharibi mwa Iraq, likichukuliwa na wapiganaji.
Eneo kubwa la ardhi kwa sasa limerudishwa, na mji wa Mosul umebakia kuwa ngome ya mwisho ya wapiganaji hao.
Ndege za Kivita za Marekani zimekuwa zikifanya mashambulizi katika mji huo, huku mjumbe maalumu wa Marekani katika Ushirika unaopambana na IS, brett McGurk akiandika katika mtandao wa Twitter kwamba Marekani inajivunia kuiunga mkono Iraq.
Kwa miezi kadhaa Iraq imekuwa ikijiandaa kufanya mashambulizi makubwa. Huku Mashirika ya haki za Binadamu yakionya kuwa raia wengi watakumbwa na maafa

NA BBC SWAHILI
Jeshi la Iraq laanza operesheni kuikomboa Mosul Jeshi la Iraq laanza operesheni kuikomboa Mosul Reviewed by habari motto on 5:12 AM Rating: 5

Wasichana wa Chibok waungana na familia zao

5:10 AM
Wasichana wa Chibok, Nigeria
Wasichana wa shule 21 ambao walitekwa na wapiganaji wa kiislamu katika mji wa Chibok hatimaye wameungana tena na familia zao.
Wasichana hao waliokuwa wakishikiliwa kwa takriban miaka miwili na wapiganaji wa Boko Haram wamesimulia mateso waliyopitia.
Mmoja wa wasichana hao anasema alidhani kuwa siku ya kuachiwa kwake haitakuja kutokea. Huku mzazi mmoja wapo akisema kwamba wanaendelea kuwaombea dua wasichana ambao bado wanashikiliwa.
Msemji wa Rais wa Nigeria Garba Shehu ameliambia Shirika la Habari la Reuters wapiganaji ambao waliwaachia wasichana hao siku ya Alhamisi bado wanawashikilia wasichana wengine wapatao 83.
Zaidi ya wanafunzi 250 kutoka Chobok walikamatwa mateka April 2014.
Wasichana wa Chibok waungana na familia zao Wasichana wa Chibok waungana na familia zao Reviewed by habari motto on 5:10 AM Rating: 5

Maandamano: Watu 10 wauawa Ethiopia

1:05 PM
Image captionMaandamano Ethiopia
Makumi ya maelfu ya watu kutoka kabila la Amharic wameshiriki katika maandamano dhidi ya Serikali nchini Ethiopia katika mji wa kaskazini wa Gondar.
Waandamanaji hao wameitaka serikali kubadilisha uamuzi wake wa kuanzisha wilaya chini ya usimamizi wa kabila la Tigray.
Serikali ya Ethiopia inasema kuwa zaidi ya watu 10 wameuawa wakati wa makabiliano na polisi kuhusu eneo linalozozaniwa katika majuma ya hivi karibuni.
NA BBC
Maandamano: Watu 10 wauawa Ethiopia Maandamano: Watu 10 wauawa Ethiopia Reviewed by habari motto on 1:05 PM Rating: 5

Jaribio la mapinduzi watu 42 wapoteza maisha Uturuki

7:04 AM
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amejitokeza katika uwanja wa ndege wa Istanbul, akiwa amezingirwa na mamia ya wafuasi baada ya kundi la wanajeshi kujaribu kupindua serikali yake.
Wanajeshi wakiwa wamesimama nje ya makao makuu
Kwenye kikao cha dharura na wanahabari, ameahidi kusafisha jeshi na akaahidi kwamba wote waliohusika wataadhibiwa vikali.
Kundi la wanajeshi lilikuwa limetekeleza jaribio la kupindua serikali.
Taarifa kutoka kwa kundi hilo la jeshi, ambayo ilisomwa kupitia runinga ya taifa ilisema jeshi lilikuwa limechukua mamlaka.
Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim ameambia runinga moja ya Uturuki kwamba hali imethibitiwa na kwamba waliohusika wataadhibiwa vikali.
Mashirika ya haabri ya serikali yanaripoti kuwa majengo ya bunge mjini Ankara yamekumbwa na mlipuko wa bomu.Kusoma zaidi bofya
Kituo cha runinga cha kibinafsi cha NTV kinasema ndege ya kivita ya wanajeshi watiifu kwa serikali imeidungua helikopta iliyokuwa ikitumiwa na wanajeshi waliotekeleza jaribio la mapinduzi mjini Ankara.
160715232127_turkey_coup_640x360_epa_nocredit
Wakati wa kutangaza mapinduzi ya serikali, kundi hilo la wanajeshi lilisema lilichukua hatua hiyo kuhifadhi utawala wa demokrasia na likatangaza amri ya kutotoka nje.
Lilisema nchi hiyo ingeongozwa na “baraza la amani” ambalo lingehakikisha utulivu na usalama.
Aidha, liliahidi kwamba utawala wa kikatiba ungerejeshwa “haraka iwezekanavyo”.
Jaribio hilo la mapinduzi ya serikali lilitekelezwa Rais Erdogan akiwa likizoni.
Alihojiwa baadaye kwenye runinga, kupitia simu na mtandao wa Facetime, ambapo alitoa wito kwa watu kujitokeza barabarani kuunga mkono demokrasia.
Jaribio la mapinduzi watu 42 wapoteza maisha Uturuki Jaribio la mapinduzi watu 42 wapoteza maisha Uturuki Reviewed by habari motto on 7:04 AM Rating: 5

AY, Iyanya, Cassper Nyovest na mastaa wengine Katika Jukwaa Moja

6:35 AM
AY Mandela
Hitmaker wa Zigo, Ambwene Yessayah aka AY ni mmoja kati ya wasanii wa Afrika watakaotumbuiza kwenye tamasha la kumuenzi Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Tamasha hilo litafanyika Jumamosi hii jijini Johannesburg.AY Mandela
Zaidi ya wasanii 20 watatumbuiza kwenye show hiyo kubwa.
CnJAY2aWYAAmo65
Wasanii wengine ni pamoja na Banky W, Iyanya, Cassper Nyovest, KCEE, Waje, Patoranking, Mtee, HHP na wengine kibao.
Nelson Mandela International Day au Mandela Day ni maadhimisho ya kila mwaka ambayo humuenzi hayati Mandela na hufanyika kila JUly 18, siku aliyozaliwa.
Siku hiyo ilianzishwa rasmi na Umoja wa Mataifa, November 2009.
AY, Iyanya, Cassper Nyovest na mastaa wengine Katika Jukwaa Moja AY, Iyanya, Cassper Nyovest na mastaa wengine  Katika Jukwaa Moja Reviewed by habari motto on 6:35 AM Rating: 5

Ujerumani yamgusia Waziri wa Uingereza

6:28 AM
Ujerumani imesema kuchaguliwa kwa Boris Johnson kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ni msimamo wa nchi hiyo, kujitoa EU.
Akizungumza kupitia televisheni ya Ujerumani, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Frank_Walter Steinmeier amesema
uamuzi uliofanywa na Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Teresa May kumchagua Johnson ni kuonesha wazi msimamo wake wa kuiongoza nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
Hata hivyo amesema anamatumaini kuwa waziri huyo mpya wa Mambo ya nje wa Uingereza atasaidia kudumisha uhusiano uliopo na Ulaya.
Boris Johnson ni mmoja ya mawaziri kadhaa wapya waliochaguliwa, ambao walikuwa wakiunga mkono nchi hiyo kujitoa Jumuia ya Ulaya.
Moja ya kazi zake za kwanza kuzifanya ni kutembelea ubalozi wa Ufaransa mjini London, kuadhimisha siku ya Bastille Day.
NA BBC SWAHILI
Ujerumani yamgusia Waziri wa Uingereza Ujerumani yamgusia Waziri wa Uingereza Reviewed by habari motto on 6:28 AM Rating: 5

Shambulizi La Kigaidi Lateketeza Zaidi Ya Watu 75 Nchini Ufaransa

6:25 AM
VALERY HACHE/AFP/Getty Images)
Shambulizi linaloaminika kuwa la kigaidi limeua zaidi ya watu 75 wakiwemo watoto huko katika mji wa Nice nchini Ufaransa. Shambulio hilo limetokea kwa mtu kuendesha gari kubwa la mizigo katikati ya watu waliokuwa wamekusanyika kuangalia fataki na kusheherekea sikukuu ya Bastille Day ambayo hulinganishwa na sikukuu ya uhuru nchini Ufaransa.
Vyombo mbalimbali vya habari vinaripoti kwamba gari hilo la mizigo lilikuwa limesheheni silaha na mabomu na kwamba dereva alianza kwanza kuwashambulia watu kwa kutumia silaha kabla ya kuanza kuwakanyaga. Aliendelea kufanya hivyo mpaka alipouawa na polisi kwa kupigwa risasi.
Tayari Rais Hollande amelielezea tukio hilo kuwa la kigaidi na ametangaza kuongeza miezi mitatu katika tangazo la hali ya hatari nchini humo.
Shambulizi La Kigaidi Lateketeza Zaidi Ya Watu 75 Nchini Ufaransa Shambulizi La Kigaidi Lateketeza Zaidi Ya Watu 75 Nchini Ufaransa Reviewed by habari motto on 6:25 AM Rating: 5

Picha Za Raisi ZUMA Na Binti Huyu Zazua Utata

6:21 AM
zuma+blesser+copy
Picha ya msichana akimbusu Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma imezua utata nchini humo.

Picha hizo zilisambaa Jumatano hii baada ya msichana huyo kuziweka kwenye mitandao ya kijamii. “We will check the matter,” alisema msemaji wa serikali Bongani Ngqulunga alipoulizwa kuhusu picha hizo.
Msichana huyo mwenye miaka 19 anaitwa Lindokuhle Dlamini. Kwenye picha hizo aliandika: He is not just a blesser, we are inlove and I am grateful for all that he has done for me, much love. Xo xo.”
Blesser inamaanisha ni mtu mzima anayehonga wasichana na kuwa na uhusiano nao. Akaunti yake ya Facebook imefutwa.
Hata hivyo mtoto wa kiume wa rais huyo, Edward amedai kuwa msichana huyo ni dada yake na kwamba akaunti iliyopost picha hizio ni feki. Baadhi ya magazeti likiwemo Citizen‚ yamesema yaliambiwa na wasomaji wake kuwa ni kweli binti huyo ni mtoto wa Zuma.
Hata hivyo Makamu wa Rais wa Economic Freedom Fighters Floyd Shivambu alikosoa kwa kutweet: Okay cool? What kind of Grand Fathers and Fathers kiss their Grand Daughters & Daughters like this? Perverts??”
Serikali bado haijatoa majibu kama ilivyoahidi.
Picha Za Raisi ZUMA Na Binti Huyu Zazua Utata Picha Za Raisi ZUMA Na Binti Huyu Zazua Utata Reviewed by habari motto on 6:21 AM Rating: 5

Lijue Baraza La Mawaziri Alilotangaza Waziri Mkuu Uingereza,Theresa May

1:37 PM
Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Theresa May amemteua Boris Johnson kuwa waziri wa Mambo ya Nje na Philip Hammond kuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo.
Aidha Amber Rudd ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Michael Fallon ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi.
Waziri Mkuu huyo mpya wa Uingereza amesema kuwa serikali yake haitanaswa na mtego wa kuwasikiliza watu walio wachache na kusahau wananchi wa kawaida. Theresa May anakuwa waziri mkuu wa 13 kuwahi kuiongoza Uingereza katika enzi ya Malkia Elizabeth wa pili.
Hapo jana waziri mkuu aliyetangaza kujiuzulu hivi karibuni, David Cameron alihutubia kwa mara ya mwisho Bunge la Uingereza na kujibu maswali ya wabunge wa Bunge hilo na baadaye aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia Elizabeth wa Pili kwenye Kasri lake lililopo huko Buckingham.
Malkia amemtaka Bi May kuunda serikali ikiwa ni historia ya pekee kwa Uingereza kupata kiongozi wa pili mwanamke baada ya Margaret Thatcher.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) wameitaka serikali ya Uingereza kuharakisha mchakato wa kujitoa rasmi katika umoja huo, lakini May amedokeza kuwa hatauharakisha mpango huo mashuhuri kwa jina la Brexit.
Changamoto kubwa inayomkabili Waziri Mkuu huyo mpya wa Uingereza ni pamoja na kuizuia Scotland inayounga mkono Umoja wa Ulaya dhidi ya kuitisha kura ya uhuru wake ili kubakia katika EU na kuimarisha mahusiano mapya ya kibiashara na kidiplomasia ili kujiandaa kwa hali ya baadaye ya baada ya kujiondoa katika umoja huo.
Lijue Baraza La Mawaziri Alilotangaza Waziri Mkuu Uingereza,Theresa May  Lijue Baraza La Mawaziri Alilotangaza Waziri Mkuu Uingereza,Theresa May Reviewed by habari motto on 1:37 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.