Wakati wajumbe wa bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakiendelea na msimamo wao wa kususia vikao vinavyotarajiwa kuanza leo mjini Dodoma hapa Tanzania, mmoja wa wajumbe wake siku ya jana aliripoti bungeni na kujiandikisha.
Mjumbe huyo, ni Clara Mwatuka ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), alionekana katika Viwanja vya Bunge saa 6:30 mchana akiwa ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo Livingstone Lusinde (Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi).
CIVIL UNITED FRONT (CUF) CHAMA CHA WANANCHI ni mojawapo ya chama kinachounda Ukawa, pamoja na Chadema na NCCR Mageuzi na tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wametangaza kwamba wajumbe wote wanaotokana na umoja wao hawatashiriki vikao vya Bunge hilo.
Mbunge huyo MH. Clara Mwatuka baada ya kujaza fomu maalumu za kujiandikisha, alielekea lango la Magharibi na kuingia kwenye gari la Mh.Jerome Bwanausi.
Mh. huyo awali , alipoulizwa kwenye Viwanja vya Bunge kuhusu kuwepo kwake Dodoma, alikataa kuzungumza lakini alikiri kujiandikisha kushiriki katika shughuli huko bungeni.
JE WAJUA....NA HUYU NDIYE MSALITI WA UKAWA
Reviewed by habari motto
on
2:43 PM
Rating: