NA HII NI TAARIFA YA CHADEMA KUHUSU WASALITI WA UKAWA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kitawachukulia hatua kali wabunge wake iliyowaita kuwa ni wasaliti kwa kupuuza maagizo ya chama na kwenda kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.


Mkuu wa kurugenzi ya sheria ya CHADEMA na msemaji wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Tundu Lissu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya chama hicho kutoa taarifa ya kuwepo njama za kutaka kukidhoofisha chama hicho.

  Kwa mujibu wa Lissu, mamlaka ya nidhamu kwa wanachama wenye hadhi ya ubunge ni kamati kuu, chombo ambacho amesema ndiyo kilichotoa maagizo ya kwamba wajumbe wote wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kutoka CHADEMA wasihudhurie vikao vya bunge maalumu la Katiba.

NA HII NI TAARIFA YA CHADEMA KUHUSU WASALITI WA UKAWA NA HII NI TAARIFA YA CHADEMA KUHUSU WASALITI WA UKAWA Reviewed by habari motto on 8:37 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.