UMEMWONA HUYU KIKWOGWE WA AJABU, AISHI KWA KULA UDONGO

Mzee aitwaye Athuman Ngusa Kulaba (80) amekuwa akiishi kwa kula udongo wa 

nyumba 

anayoishi kwa sababu ya kukosa chakula cha kibinadamu.

Kikongwe huyo alikutwa hivi karibuni nyumbani kwake, Chanika wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam baada ya majirani kusema kwamba wamekuwa wakimshuhudia akipata mlo huo kwa karibu mwaka mmoja sasa.


Baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, mjumbe wa eneo hilo, John Kanguya na majirani  zake walimchukuwa hadi kwenye Kituo cha Afya cha Chanika kwa ajili ya kumpima afya yake ambapo madaktari walisema tayari alipatwa na ugonjwa wa safura ambapo tumbo lake limejaa minyoo.
Alisema anawashukuru majirani wa eneo hilo ambao wameweza kutambua maisha magumu anayoishi na kuamua kumpeleka hospitali na kumsaidia chakula.
 Kwa sasa naomba Watanzania wenzangu wanisaidie nauli ili niweze kurudi kwetu Bukene, Tabora, maisha hapa ni magumu sana
alisema kikongwe huyo.
Kwa Watanzania watakaoguswa na maisha magumu ya mzee huyo wanaweza kumsaidia nauli kwa kutumia namba ya simu ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Chanika, Mohamed Katungi 0784 295833 au 0715 295833.
UMEMWONA HUYU KIKWOGWE WA AJABU, AISHI KWA KULA UDONGO UMEMWONA HUYU KIKWOGWE WA AJABU, AISHI KWA KULA UDONGO Reviewed by habari motto on 11:15 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.