Miongoni mwa watu ambao nimegundua wana utani na utaenjoy kukaa nao ni pamoja na Fid Q, Mr. Blue, Baba Levo, Msechu na hayo ni baadhi tu lakini kuna wengine wana vituko vyao vya kipekee kama Raymond wa Tiptop Connection ambae mara nyingi huonekana kwenye stage na Madee ambapo wakati anamuigilizia Nay hakuwepo.
Raymond ambae pia ni mchekeshaji na mtani alionyesha uwezo wake kwenye kuigiza sauti ya Nay wa Mitego wakati Tour ya Fiesta ilipotua Mbeya (87.8 CloudsFM) ambapo ukishaisikiliza unaweza kuniachia comment yako kuniambia amempatia kwa asilimia ngapi?

Miongoni mwa wasanii ambao walichekeshwa sana na utundu huu wa Raymond ni pamoja na Mr. Blue, T.I.D, Linah, Linex na wengine ambao sauti zao wakicheka na kuongea zinasikika kwa mbali.
Hii pia ilikua ni siku nyingine ambapo Chege alichukua mic ya CloudsTV na kuanza kuhoji Wakali wengine ndani ya basi, Ommy Dimpoz, Blue, Mh. Temba ni watu wengine poa sana kukaa nao
Hiki kipaji si Mchezo..Sikia Jinsi Raymond wa Tip TOP akiigiza saut ya Ney Wa Mitego
Reviewed by habari motto
on
2:00 PM
Rating: