Tofauti na mastaa wengine ambao huandika majina ya wapenzi wao kwenye
miili yao kuonesha jinsi wanalivyo na mapenzi nao, Nasibu Abdul
‘Diamond’ na Wema Sepetu wamekuwa tofauti.
Mastaa hawa wameonyesha kuwa na mapenzi na wazazi wao ambapo
mwandishi wetu amebaini Diamond ameandika jina la mama yake mkononi huku
Wema akiandika jina la baba yake mkononi pia.
Wote wamefanya hivyo kwenye mikono yao ya kushoto sambamba na uwepo
wa tatoo nyingine ambapo Wema ameandika ‘Daddy Sepetu’ na Diamond
akaandika Sandra…’
Tattoo ya Wema Sepetu ikionekana kwenye mkono wake wa kushoto. Hata
hivyo, baadhi ya mashabiki wao wamedai huenda penzi la mastaa hao si la
kudumu ndiyo maana wamekwepa kuandikana ili isije ikawa shida pale
watakapomwagana.
Shuhudia Wema na Diamond Walivyowaenzi Wazazi Wao
Reviewed by habari motto
on
12:38 PM
Rating:
Reviewed by habari motto
on
12:38 PM
Rating:

