.jpg)
WAKATI bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya kuzomewa na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita, Wema Sepetu ‘Madam’ anaponda raha ya maisha nchini China, Amani
lina full data. Chanzo makini kilicho ‘kloz’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini, kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache kabla ya Tamasha la Fiesta, akiwa ameandamana na wanaume wawili, ambao ni meneja wake, Martin Kadinda na Petit Man, wote wakiwa wamekaa daraja la kwanza la dege hilo.
.jpg)
Chanzo hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo
zilibebwa na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la
Guangzhou nchini humo, Wema na wanaume hao wawili walichukua
vyumba katika Hoteli ya Holiday Inn, inayotajwa kuwa moja ya hoteli
ghali zaidi huko China.
“Yaani Wema jamani ana mambo, inavyoonekana lile rhumba la wakati
ule ameshalisahau, amesahau kabisa kama alishafulia, sasa Mungu
kamjaalia kapata pesa anavyoitapanya ovyo mpaka roho inauma. Wewe
fikiria mtu amekwenda kuchukua vifaa vya biashara, unakwenda na hao
wanaume wa kazi gani kama siyo kupoteza fedha tu,” kilisema chanzo
hicho.
Inadaiwa kwamba kilichompeleka Wema katika nchi hiyo yenye watu
wengi zaidi kuliko yoyote duniani, ni ununuzi wa vipodozi, kwani ana
mpango wa kufungua duka kubwa katika eneo ambalo halijatajwa jijini
Dar es Salaam.
Baada ya kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu
wamekuwa wakiishi maisha ya starehe, wakila bata katika klabu
mbalimbali za usiku, ambako wanajichanganya na watanzania wengine
kuponda raha.
“Kwa matanuzi anayofanya kule, hata hiyo biashara aliyoifuata haina
maana, angekuwa mtu mwenye nia ya biashara kweli, angetafuta tu
hoteli ya kawaida ili kubana matumizi aweze kuja na mzigo mkubwa,
sasa wewe mwenyewe fikiria, hii wiki ya pili sasa, tena na wanaume
wawili wanakutegemea, hizo pesa si kuzitapanya tu jamani,” kilisema
chanzo hicho kikionyesha kutofurahishwa na maisha ya staa huyo.
GPL
Wema Sepetu Aponda Raha China Huku Platinums Akiugulia Machungu
Reviewed by habari motto
on
9:25 AM
Rating:
Reviewed by habari motto
on
9:25 AM
Rating: