Meli vita ya Indonesia KRI Yos Sudarso moja ya meli kadhaa zinazoshiriki usakaji wa ndege ya AirAsia .
WATAALAMU wanaosaka ndege ya AirAsia yenye mruko namba QZ8501 wamesema wameona mabaki ya ndege hiyo kwa kutumia utaalamu wa kusikia mshindosauti (sonar) chini ya bahari ya Java.
Hata hivyo taarifa waliyoitoa dakika 40 zilizopita wamesema kwamba hawana uhakika kama ndege hiyo ipo nzima au ni kipande tu kimeonekana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ndugu wa abiria waliokuwapoi katika ndege hiyo wametaarifiwa kuonekana kwa mabaki hayo.
Awali jana watafutaji hao waliona sehemu ya mabaki yakielea.
Aidha maiti kadhaa zilizpatikana jana.
Mabaki hayo yalipatikana umbali wa kilomita 100-200 kutoka eneo la mwisho ambalo rubani alifanya mawasiliano ya kutaka kubadili njia.
BREAKING NEWS: Mabaki ya ndege AirAsia yaonekana chini ya bahari
Reviewed by habari motto
on
9:58 AM
Rating: