Ukifika nje ya geti la Kituo cha Masanga tangu mwezi huu wa 12 ulipoanza utakutana na huu ujumbe ''HAKATWI MTU HAPA'' hiki ni kituo cha kuzuia ukeketaji (TFGM) ambacho kinatoa mafunzo ya ukeketaji mbadala na tohara salama... kwa sasa kuna watoto zaidi ya 600 ambao wamekimbilia hapa ili wasikeketwe tangu msimu huu ulipoanza mwezi wa 12/2014...
Mwezi wa 12 ni mwezi wa kufanya tohara mkoani Mara ambapo watoto wengi huwa wamefunga shule na hivyo kupelekea watoto wa kike hukeketwa...
Mwezi wa 12 ni mwezi wa kufanya tohara mkoani Mara ambapo watoto wengi huwa wamefunga shule na hivyo kupelekea watoto wa kike hukeketwa...
Pata mwonekano wa Kituo cha Masanga, ambacho kipo katika kijiji cha Masanga Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara...
Kituo hiki cha Masanga kinategemea sana maji ya mvua, na mvua hazijanyesha siku za karubuni, jmosi iliyopita waliletewa maji na Mkuu wa Wilaya ya Tarime.... kwa hiyo wanahitaji msaada wa haraka sana sana...
Mabango haya yamebeba ujumbe tofautitofauti kwa lengo la kuifikishia jamii kilio chao kutokana na hii mila yao ya Ukeketaji...
Niliwatia moyo kwamba wakati mwingine inabidi wasisubiri kufanyiwa MAAMUZI hasa yale maamuzi yenye madhara kama hii mila ya Ukeketaji...
Watoto waliokimbilia kituo cha Masanga kujiokoa na kisu cha msumu huu wa Ukeketaji mkoani Mara...
Watoto zaidi ya 600 wakitoa sauti zao kupinga kukeketwa mwezi huu wa 12/2014.. wanahitaji msaada wa dharura kama Maji, chakula, pedi, n.k
Watoto wakitoa sauti zao nje ya kituo cha Masanga kuieleza jamii ya Tanzania na Dunia nzima juu ya Mila yao ya Ukeketaji ambayo inawakandamiza wasichana kwa kiasi kikubwa...
Hivi Ndivyo Maandamano Kupinga Ukeketaji Yalivyoteka Hisia
Reviewed by habari motto
on
4:13 PM
Rating: