Pancho Mwamba Akanusha Kufumaniwa Na Kupigwa

Patcho Mwamba akiwa katika ofisi za Global Publishers Ltd leo.
Patcho akipozi na mwandishi Nyemo Chilongani wa Global.
Picha ya Patcho iliyozua utata mitandaoni.
MWIGIZAJI na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba hivi punde ameibuka katika ofisi za mtandao huu na kukanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
Akiongea na mtandao huu, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.
"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe
juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho akiwa katika ofisi za mtandao huu zilizopo Mwenge-Bamaga, Dar.
Pancho Mwamba Akanusha Kufumaniwa Na Kupigwa Pancho Mwamba Akanusha Kufumaniwa Na  Kupigwa Reviewed by habari motto on 8:23 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.