Ridhiwani Afanya Ziara Jimboni Chalinze

 Ridhiwani Kikwete,(katikati ),mwenye shati nyeupe akiambatana na wafanyabiashara wa soko la Chalinze katika kuhakiki mipaka ya eneo la ujenzi wa soko hilo ambalo linadaiwa kumegwa na baadhi ya watu kwa kujengwa nyumba yao.Ridhiwani alifanya ziara hiyo mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kutaka kutatua changamoto hiyo kwa kujenga soko la kisasa.

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze(CCM) Ridhiwani Kikwete,akiwasihi madereva wa bodaboda waliopo katika jimbo hilo kutuliza hasira kutokana na mmoja wao kukamatwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kuchochea vurugu zilizosababisha mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki kupigwa na kuchomwa moto hadi kufa,tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita jimboni humo.

Ridhiwani Kikwete ,wa kwanza kushoto akikabidhiwa dhana za kimila na wazee wa Kijiji cha Msoga ikiwa ni sehemu ya kumkaribisha rasmi katika Kijiji hicho hafla hiyo ilifanyika jana kijijini hapo ,picha na Gustaphu Haule
Ridhiwani Afanya Ziara Jimboni Chalinze  Ridhiwani Afanya Ziara Jimboni Chalinze Reviewed by habari motto on 4:42 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.