Askari Polisi Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha, Baada Ya Kufanya Unyama Huu

Gilbert Ingosi Chemoso
AFISA wa Polisi aliyemnyang’anya mfanya biashara KSh90,000 punde tu alipozitoa benki Alhamisi alihukumiwa kunyongwa na hakimu mkuu katika  Mahakama ya Milimani,  Nairobi Bi Hannah Ndung’u.
Bw Crispin Odongo alishambuliwa na wezi punde tu alipotoka ndani ya benki ya Barclays tawi la Viwandani Nairobi. Alitiwa pingu na Konstebo Gilbert Ingosi Chemosi kabla ya kumsukumwa na kumwigiza ndani ya gari lililokuwa na majambazi.

Gari lililichomoka mbio.
“Hii mahakama imekupata na hatia ya wizi wa mabavu ukiwa umejihami na bunduki ya AK 47. 

Ukishirikiana na wengine mlimnyanng’anya Bw Odongo Sh90,000 na simu muundo wa Tecno yenye thamani ya Sh3,500. Utanyongwa kwa mujibu wa sheria,”akaamuru Bi Ndung’u.

Mahakama ilikashifu vikali tabia ya afisa huyo kugeuka kuwa mwizi kinyume cha kiapo cha maafisa wa usalama cha kuwalinda na kuwatunza wananchi na mali zao.

Bi Ndung’u alisema mshtakiwa huyo alikutwa na seti ya pingu katika makazi yake na kushangaa “ alikuwa anafanya nazo nini ndani ya nyumba yake kama sio za kutumika kutekeleza uhalifu.”

Konstebo Chemosi alikuwa anahudumu katika kituo cha polisi cha Makongeni na alipotekeleza wizi huo alikuwa amepelekwa kulinda benki ya Credit Bank Ltd iliyoko barabara ya Bandari eneo la  Viwandani kaunti ya Nairobi.

Ushahidi wakosekana
Huku Konstebo Chemosi mwenye umri wa miaka 38 na ambaye ametumikia kikosi cha polisi miaka 23 akienda kutiwa kitanzi mshukiwa mwingine waliyekuwa wameshtakiwa pamoja aliachiliwa huru kwa kukosekana ushahidi.

Bw George Kamau Ndogo alitabasamu alipoachiliwa lakini uhuru wake haukuwa wa muda mrefu kwani aliondolewa seli na kupelekwa mbele ya hakimu mwandamizi Joseph Karanja katika mahakama hiyo hiyo ya Milimani kuendelea na kesi nyingine dhidi yake ya wizi.

Wote wawili Konstebo Chemosi na Bw Ndogo walikabiliwa na shtaka la kumnyang’anya kimabavu Bw Crispin Odongo Sh90,000 na simu ya rununu muundo wa Tecno yenye thamani ya Sh3,500 mnamo Juni 25 2012.

Walishtakiwa kuwa walikuwa wamejihami kwa bastola na bunduki aina ya AK47 walipompora Bw Odongo pesa na simu. Walidaiwa walikuwa wameshirikiana na majambazi wengine walipotekeleza uhalifu huo.

Konstebo Chemosi alikabiliwa na shtaka la pili la kukataa akichukuliwa alama zake za vidole na maafisa wa upelelezi Sajini John Shegu na Koplo Jairus Mbondo alipotiwa nguvuni mnamo Mei 25, 2013.

Akipitisha hukumu, Bi Ndung’u alisema Chemosi alitekeleza wizi huo mchana saa nane kasoro dakika kumi katika barabara ya Bandari eneo la Viwandani Nairobi.

“Chemosi alitambuliwa  kabisa na Bw Odongo kwa vile ndiye alimtia pingu na kumsukuma kwa nguvu  na kumwigiza ndani ya gari lililokuwa na wezi waliochomoka mbio kama gari la Safari rally,” Bi Ndung’u alisema akipitisha hukumu.

Pia Chemosi alitambuliwa tena na Bw Odongo wakati paredi iliyofanywa kumtambua afisa aliyehusika na wizi huo.

Alipewa siku 14 kukata rufaa.
Askari Polisi Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha, Baada Ya Kufanya Unyama Huu Askari Polisi Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha, Baada Ya Kufanya Unyama Huu Reviewed by habari motto on 11:41 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.