Results for "EAST AFRICA"

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda

6:57 AM
Image result for Robert Kyagulanyi
Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi saa kadhaa baada ya dereva wake kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Awali Bobi Wine alidai kuwa dereva wake aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari lake.
Mbunge huyo wa Kyadondo aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa walikuwa eneo linalojulikana kama Arua kwenye kampeni wakati mauaji hayo yalitokea.
Uchaguzi mdogo unatarajiwa kuandaliwa eneo hilo siku ya Jumatatu katika juhudi za kumtafuta yule atakayechukua mahala pake mbunge aliyeuawa Ibrahim Abiriga .
Bobi Wine na viongozi kadhaa wa upinzani walikuwa eneo hilo kumuunga mkono mgombea huru Kassiano Wadri.
Mikutano hiyo ilienda sawa siku yote kabla ya polisi kuanza kukabiliana na wafuasi wa Wadri.
Wafuasi wa Wadri nao waliripotiwa kukabiliana na wale wa mgombea wa NRM Tiperu Nusura.
Bobi Wine pia aliandika kuwa hoteli yake ilizingirwa na polisi kufuatia visa hivyo.
Hata hivyo polisi wanasema kuwa wafuasi wa upinzani watalaumiwa kwa kuuliwa dereva huyo wa Bobi Wine Yasin Kawuma.
Msemaji wa polisi Emilian Kayima, anasema watu waliokuwa wamevaa shati za kampeni za mgombea Wadri, walianza kuurushia mawe msafara wa rais hali ambayo ilisababisha polisi kufyatua risasi.
"Mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni msafara wa rais ulishambuliwa na wahuni katika manispaa ya Arua wakati rais alikuwa anaondoka uwanja wa Boma ambapo alikuwa amefanya mkutano wa mwisho," Kayima alisema.
Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda Reviewed by habari motto on 6:57 AM Rating: 5

Ni Raila Odinga! Hongereni NASA

6:46 AM





Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, NASA, umemteua Mhe. Raila Odinga kuwa mgombea Urais na Kalonzo Musyoka kuwa Naibu Rais. Mwezi uliopita nilipokuwa Nairobi nilikutana na kuzungumza na Mhe. Raila kwa Dakika kadhaa kwenye Mkutano wa Vyama vya Kiliberali barani Afrika . Lakini nilipata fursa ya kushiriki naye katika kundi kazi la viongozi wachache kwa siku nzima. Raila alinihakikishia kuwa NASA haitavunjika, leo nashuhudia kauli yake ikiwa ukweli mtupu. NASA has spoken it clearly, it is Raila Odinga! Hongereni NASA!
Ni Raila Odinga! Hongereni NASA Ni Raila Odinga! Hongereni NASA Reviewed by habari motto on 6:46 AM Rating: 5

Sudan Kusini Yajiunga E.A.C

2:16 AM
sam1
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa  wakimsubiri  Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016.
sam3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016, Kushoto ni Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
sam5
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit akikagua gwaride la heshima  wakati Rais Kiir   alipowasili Ikulu leo.
sam6
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir akiwapungia mikono viongozi mbalimbali huku akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakati alipowasili Ikulu
sam7
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki CEAC) na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir wakibadilishana hati za makubaliano ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kusaini 
sam8
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir. Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo ya utiaji saini.
Sudan Kusini Yajiunga E.A.C Sudan Kusini Yajiunga E.A.C Reviewed by habari motto on 2:16 AM Rating: 5

‘Waliompinduwa’ Nkurunziza Wafugwa Kifungo cha Maisha

6:47 AM
Generali Ndayirukiye mmoja wa wanamapinduzi wa Pierre Nkurunziza
Genrali Ndayirukiye mmoja wa wanamapinduzi wa Pierre Nkurunziza
MAHAKAMA nchini Burundi imewahukumu kifungo cha maisha majenerali wa jeshi walioongoza mapinduzi dhidi ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. Mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine tisa miaka 30 jela kwa kitendo cha kuhusika katika jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi.
Wanne kati ya hao watakaotumikia kifungo cha maisha jela ni aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Cyrille Ndayirukiye, Jenerali Zenon Ndabaneze, Juvenal Niyungeko na Hermenegilde Nimenya aliyekuwa Kamishana wa Polisi.
Awali upande wa mashtaka uliiomba mahakama kuwafunga washtakiwa wote kifungo cha maisha baada ya kukiri kushiriki katika jaribio hilo la mapinduzi mnamo mwezi Mei.
BBC
‘Waliompinduwa’ Nkurunziza Wafugwa Kifungo cha Maisha ‘Waliompinduwa’ Nkurunziza Wafugwa Kifungo cha Maisha Reviewed by habari motto on 6:47 AM Rating: 5

Rais Kagame Awapa Mbinu Viongozi wa Burundi Kutafuta Suluhu

8:27 PM
Rais wa Rwanda Paul Kagame amewashauri raia wa Burundi kumaliza mgogoro unaoendelea nchini humo kwani hakuna mtu wa nje anayeweza kufanya hivyo.

Rais Kagame alisema kuwa, viongozi na nchi hiyo na raia hao wana wajibu wa kushughulika na mambo yao ya ndani kuliko kutegemea msaada wa watu wengine.

“Siyo kweli kwamba Rwanda inafurahia mgogoro wa kisiasa unaoendelea Burundi kwani athari zake zinatugusa hata huku. Wakimbizi wanazidi kuongezeka hivyo ni vyema wakatafuta ufumbuzi haraka iwezekanavyo kuyanusuru maisha ya watu,” alisema.

Kiongozi huyo alikanusha uvumi kwamba nchi yake imekuwa ikisaidia baadhi ya makundi ya wapiganaji yanayopingana na Serikali ya Burundi.

“Hayo ni madai ya yasiyo ya kweli na kama kuna mwenye ushahidi kuhusu hilo athibitishe. Huu siyo wakati wa lawama kwani jambo la muhimu ni suluhu itakayomaliza mgogoro huo,” alisema.



Amuunga mkono Museveni

Katika hatua nyingine, Kagame alionyesha kumuunga mkono Rais wa Uganda Yoweri Museveni anayewania madarakani kwa muhula wa tano.

“Ukiniuliza mtazamo wangu kuhusu Uganda jibu ni kwamba nimefanya kazi vizuri na viongozi waliopo madarakani hivyo nawatakia kila la heri kwenye uchaguzi ujao,” alisema na kuongeza kuwa:

“Naamini waganda ni watu wenye akili timamu na uelewa wa kutosha utakaowawezesha kufanya uchaguzi sahihi bila kuleta machafuko katika nchi yao.”

Kuhusu uamuzi ambao mataifa ya magharibi yanaweza kuchukua kutokana na kufanyika mabadiliko Katiba ya Rwanda, Kagame alisema Warwanda hawawezi kuishi kwa kufuata matakwa ya watu wengine.

“Wanyarwanda wataishi wanavyotaka. Hatuwezi kuwa waoga na watiifu kupita kiasi kwa vile tunategemea misaada kutoka kwa wahisani, binafsi sidhani kama kuna matatizo makubwa yanayoweza kutokea na yakawa zaidi ya yaliyowahi kutukuta,” alisema.


Uamuzi wa bunge

Juzi, Bunge la Burundi lilipinga mpango wa Umoja wa Afrika wa kutaka kutuma kikosi cha kusimamia amani katika nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa.

Spika wa Bunge hilo, Pascal Nyabenda alisema hakuna dharura ya kutuma kikosi cha umoja huo nchini humo.

Kwa upande wake, Spika wa Baraza la Seneti la Burundi, Reverien Ndikuriyo alisisitiza kuhusu tofauti baina ya mauaji na mauaji ya kimbari.

Wabunge na wawakilishi wa baraza hilo wakiwa katika kikao chao, walikubaliana kwamba Serikali ifanye kila iwezalo kukomesha mauaji yanayohatarisha amani nchini humo.

Ijumaa iliyopita Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika llilipitisha uamuzi wa kupeleka kikosi cha askari 5,000 nchini humo.

Kabla ya hatua hiyo ya Bunge na Baraza la Seneti, Msemaji wa ofisi ya Rais alikuwa ametoa radiamali yake kuhusiana na uamuzi wa Umoja wa Afrika wa kutaka kutuma kikosi cha kusimamia amani Burundi na kutangaza kuwa, endapo AU itatuma kikosi hicho na kupuuza upinzani wa Serikali kwa hatua hiyo, vikosi hivyo vitahesabiwa kuwa ni majeshi vamizi.

Viongozi wa Serikali wanadai kuwa vitendo vya utumiaji mabavu vya vikosi vya usalama vinafanyika katika fremu ya kurejesha amani na usalama, wapinzani wanasema kuwa, hatua hizo ni za ulipizaji kisasi dhidi yao na lengo lake ni kuwauwa wapinzani wa serikali.

Katika hali ambayo, weledi wengi wa masuala ya kisiasa wanatahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea vita vya ndani na kuanza mauaji mengine ya kimbari Burundi, Umoja wa Afrika umetangaza kuwa hautaruhusu kuanza vita na kutokea mauaji mengine ya kimbari barani humo.

Waziri wa Ulinzi wa Uganda, Crispus Kiyonga ambaye nchi yake ni mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mgogoro wa Burundi alitangaza hivi karibuni kwamba, njia bora kabisa katika mazingira ya hivi sasa na hali ya usalama inazidi kudorora nchini humo ni kuanza mazungumzo kwa minajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Kiyonga alisema, viongozi wana mambo 10 ambayo wanataka yatiwe katika ajenda ya mazungumzo ya tarehe 28 Desemba.

Miongoni mwa mambo hayo ni utawala wa awamu ya tatu ya uongozi wa Rais Pierre Nkurunziza, jedwali la uchaguzi, hali ya usalama pamoja na serikali ya umoja wa kitaifa.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha, zaidi ya watu 240 wameuawa na zaidi ya 200,000 wakilazimika kuyakimbia makazi yao, kutokana na machafuko hayo tangu Aprili mwaka huu.

Machafuko hayo yalitokea baada ya chama tawala CNDD-FDD kumwidhinisha Rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa muhula wa tatu mfululizo.

Wapinzani Burundi walisema, hatua ya Nkurunziza kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliopita ilikuwa kinyume na katiba.
Rais Kagame Awapa Mbinu Viongozi wa Burundi Kutafuta Suluhu Rais Kagame Awapa Mbinu Viongozi wa Burundi Kutafuta Suluhu Reviewed by habari motto on 8:27 PM Rating: 5

Baraza la Mawaziri Kenya, labadilishwa

7:02 AM
Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, na kuwaacha wote wizara zao zilizotajwa katika ufisadi.
Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa. Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni.
Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni,Rais Uhuru Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka kumi na tisa hadi ishirini na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora zaidi.
Idara hizo zimeongezwa kutoka ishirini na sita hadi arobaini na moja.
Rais Kenyatta amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri baada ya mawaziri sita kulazimika kujiondoa kutokana na wizara walizosimamia kuhusishwa na ufisadi huku wawili kati yao wakikabiliwa na kesi mahakamani.
Ni Mabadiliko yaliyotarajiwa hasa baada ya hatua ya aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru kujihuzulu mwishoni mwa juma kutokana na kile alichosema ni ushauri wa daktari wake- baada ya usumbufu aliopata wizara yake ilipohusishwa na sakata kadhaa za ufisadi.
Kwa mujibu wa katiba idadi ya mawaziri inapaswa kuwa kati ya kumi na wanne na ishirini na wawili- na hivyo kujiuzulu kwake kulisababisha idadi hiyo kupungua hadi kumi na tatu.
Baraza jipya la mawaziri linajumuisha wanawake wanne na wanaume kumi na sita.
Baadhi ya mawaziri wamesalia katika nafasi zao huku wengine wapya wakiteuliwa kuchukua nafasi za mawaziri waliohusishwa na ufisadi.
Hatua itakayofuata sasa ni kwa mawaziri wapya kuchunguzwa na kamati ya bunge kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.
Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imekuwa ikikabiliwa na changamo ya ufisadi katika wizara kadhaa na kumekuwepo shinikizo sio tu kutoka kwa wananchi lakini pia kutoka kwa mashirika ya kijamii,viongozi wa upinzani na hata mabalozi wa nchi za kigeni kutaka hatua zichukuliwe.
Baraza la Mawaziri Kenya, labadilishwa Baraza la Mawaziri Kenya, labadilishwa Reviewed by habari motto on 7:02 AM Rating: 5

Uchumi Kufunga Maduka Yake Tanzania Na Uganda

1:59 AM

Maduka ya jumla ya Uchumi yametangaza kufungwa kwa oparesheni zake nchini Tanzania na Uganda katika zoezi la kubana matumizi

Mkurugenzi mkuu wa maduka hayo Dr.Julius Kipng'etich amesema kuwa bodi yake imeamua kufunga vituo hivyo kwa lengo la kutathmini muundo wa oparesheni zake nchini Kenya. ''Maduka yetu nchini Tanzania na Uganda yanajumlisha asilimia 4.75 ya oparesheni zetu licha ya kutugharimu asilimia 25 ya oparesheni zetu''.

Maduka ya uchumi katika mataifa hayo mawili hayajazalisha faida yoyote katika kipindi cha miaka 5 swala ambalo linalazimu faida zinazopatikana katika maduka ya Kenya kutumika,alisema Kipng'etich.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari maduka hayo yameandika barua kwa Mamlaka ya masoko nchini Kenya ,soko la hisa pamoja na washikadau muhimu kuhusu uamuzi huo na kuongezea kwamba hivi karibuni uchumi itahitaji kuungwa mkono na wamiliki wa hisa ili kuidhinisha mpango huo.

Maduka yote katika mataifa hayo mawili yamefungwa.
via BBC Swahili
Uchumi Kufunga Maduka Yake Tanzania Na Uganda Uchumi Kufunga Maduka Yake Tanzania Na Uganda Reviewed by habari motto on 1:59 AM Rating: 5

Wakenya kumpokea Obama Kwa Stail Ya Utofauti Kabisaa

6:31 AM

Kundi la Wakenya, limejiapiza kumkaribisha rais wa Marekani, Barack Obama, nchini kwao wakiwa hawajavaa nguo ili kuonesha kuwa hawajakubaliana na kitendo cha kuruhusu mapenzi ya jinsia moja.
 
Obama anatarajiwa kutembelea Kenya kwa mara ya kwanza tangu kuwa rais na kutegemea kuwa na mkutano na wafanyabiashara kuanzia Julai 24-26 mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa barua iliyosambazwa na kundi hilo la wakenya, imedai kuwa watafanya maandamano ya amani jijini Nairobi, Julai 22 na 23 mwaka huu kuanzia Uhuru kona.
 
Wamedai kuwa maandamano hayo yatafanywa na wanawake pia wanaume takriban 5,000 wakiwa watupu bila nguo yoyote kupinga Umoja wa nchi za Amerika kupitisha sheria ya mashoga kutambuliwa kisheria.
 
Wamesema lengo kuu la maandamano wakiwa uchi ni kumuonesha na kuelewesha rais Obama, utofauti uliopo kati ya wanawake na wanaume.
 
Wiki iliyopita, Wakenya hao walienda katika mitaa kuandamana wakimuonya rais Obama, kutothubutu kuzungumzia suala la haki za mashoga kwenye ziara yake ya kutembelea nchi hiyo.
 
Mbunge Charles Njagagua, pia aliwataka wabunge kumfukuza Obama, nje ya Bunge mara moja akigusia haki za mashoga.
 
Naye Makamu wa rais nchini Kenya, William Ruto, hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wananchi wake kuwa wamesikia kuwa Marekani wameruhusu uhusiano wa mashoga na mambo mengine yasiyo na maadili na kuwataka viongozi wa dini kutetea nchi yao na kusimamia imani ya nchi yao.
Wakenya kumpokea Obama Kwa Stail Ya Utofauti Kabisaa Wakenya kumpokea Obama Kwa Stail Ya Utofauti Kabisaa Reviewed by habari motto on 6:31 AM Rating: 5

Rais Nkurunziza alivyofika Kupiga kura kwenye Uchaguzi leo June 29 2015 Burundi.

7:13 PM
Burundi
June 29 2015 Burundi wanafanya Uchaguzi Mkuu leo, lakini ishu ni kwamba Uchaguzi huo wa Wabunge unafanyika huku vyama vya Upinzani wakiwa wamesusia Uchaguzi huo.. kingine ni kwamba japo kumekuwa na machafuko ya muda mrefu kupinga RaisPiere Nkurunziza kugombea kwa mara ya tatu kwenye Uchaguzi huo lakini Ratiba inavyoonesha ni kwamba Uchaguzi wa Rais utafanyika mwezi July 2015.
Leo umefanyika Uchaguzi wa Wabunge, picha zilizoenea Mitandaoni zinamwonesha Rais Nkurunziza akiwa anaelekea kupiga kura akitumia usafiri wa baiskeli.
Piere II
Piere III
Piere
Burundi II
Pembeni ya vituo vya Kupigia kura walikuwepo Askari wakiwa na silaha kuhakikisha Usalama unakuwepo.
Rais Nkurunziza alivyofika Kupiga kura kwenye Uchaguzi leo June 29 2015 Burundi. Rais Nkurunziza alivyofika Kupiga kura kwenye Uchaguzi leo June 29 2015 Burundi. Reviewed by habari motto on 7:13 PM Rating: 5

Rais Kagame ayakosoa vikali madola ya Magharibi

9:26 AM


Rais Paul Kagame wa Rwanda amezikosoa nchi za Magharibi kwa hatua ya kumtia mbaroni Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya nchi yake huko Uingereza. 

Rais Kagame ameelezea ukosoaji wake huo katika hotuba aliyoitoa mbele ya Bunge la Rwanda hii leo na kusema kuwa, kitendo cha kumtia mbaroni Jenerali Karenzi Karake, Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya nchi hiyo kuwa ni cha kulidhalilisha taifa lake. 

Rais Kagame amesema kuwa, huwenda maafisa wa Uingereza walimfananisha Jenerali Karake na wahajiri haramu na ndio maana wakamtia mbaroni na kusisitiza kuwa, Wamagharibi wanamchukulia kila mtu mweusi kuwa ni mhajiri haramu. 

Amesisitiza kuwa, siku zote watu weusi katika nchi za Kimagharibi wanakumbwa na ukandamizaji na ukatili kutokana na wao kuwa weusi.

Karenzi Karake mwenye umri wa miaka 54 alifikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya Westminster baada ya kukamatwa kufuatia waranti uliotolewa na jaji wa mahakama ya Uhispania, Fernando Andreu, kwa madai ya kuhusika katika jinai za kivita dhidi ya raia. 

Kutiwa mbaroni Karake kumeibua hasira kali kwa serikali ya Rwanda. Kwa mujibu wa serikali ya Kigali, kutiwa mbaroni afisa huyo wa usalama kumefanyika kwa sababu za kisiasa.

Rais Kagame ayakosoa vikali madola ya Magharibi Rais Kagame ayakosoa vikali madola ya Magharibi Reviewed by habari motto on 9:26 AM Rating: 5

Burundi kuendelea na ratiba ya uchaguzi

9:25 AM
Serikali ya Burundi imesema haitashiriki katika mazungumzo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakilenga kupunguza hali ya uhasama uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenye utata.
Waziri wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana, amsema ratiba ya uchaguzi haitabadilika.
Maandamano yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadha kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania nafasi ya urais kwa mara ya tatu.
Viongozi wawili katika serikali ya Rais Nkurunziza - akiwemo mmoja wa makamu wa rais, Gervais Rufyikiri, na spika wa bunge la nchi hiyo, Pie Ntavyohanyuma, wamekimbilia Ubelgiji.
Wote wawili wamekuwa wakosoaji wa rais. Uchaguzi umepangwa kufanyika mwezi uajao. Uchaguzi wa wabunge unafanyika Jumatatu.
NA BBC SWAHILI.
Burundi kuendelea na ratiba ya uchaguzi Burundi kuendelea na ratiba ya uchaguzi Reviewed by habari motto on 9:25 AM Rating: 5

Makamu wa rais Burundi atoroka

2:31 PM

Makamu wa rais Burundi anaaminika kuwa ametorokea Ubeljiji

Moja kati ya makamu wa rais wa Burundi ametoroka nchini humo baada ya kutangaza kuwa anapinga hatua ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Makamu wa pili wa Rais wa Burundi Gervais Rufikiri amekimbia baada ya kuiambia runinga ya France24 kuwa muhula huo wa tatu unakiuka sheria na katiba ya taifa hilo.

null
Rais Nkurunziza alitibua mzozo baada ya kutangaza kuwania muhula wa tatu

Msemaji wa serikali hata hivyo amekanusha madai hayo na kusema kuwa bwana Rufikiri amesafiri nje kwa ziara rasmi ya kikazi.
Bwana Rufikiri amesema amekimbilia usalama wake akidai kuwa maisha yake yamo hatarini.
Msemaji huyo wa serikali amesema iwapo bwana Rufikiri ametoroka Burundi ni kwa maslahi yake mwenyewe wala hakuna yeyote aliyemtishia maisha yake.

null
Umoja wa mataifa unaendelea na jaribio la kuwapatanisha mahasimu Burundi

Kutoroka kwake kunafwatia kutoroka kwa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na jaji mmoja wa mahakama ya kikatiba.
Burundi imekumbwa na mzozo wa kisiasa tangu rais Nkurunziza atangaze hamu ya kuwania muhula wake wa tatu uongozini.
Wapinzani wake wanasema kuwa muhula huo wa tatu unakiuka katiba ya taifa.

null
Uchaguzi nchini humo umeratibiwa kufanyika Julai tarehe 15

Kwa upande wake rais Nkurunziza anashikilia kukutu kuwa kulingana na makubaliano ya kusitisha vita ya Arusha, muhula wa kwanza aliochaguliwa na viongozi na wajumbe waliowakilisha majimbo hakuchaguliwa na umma kama inavyoelezewa na katiba ya nchi hiyo.
Kufikia sasa makundi ya upinzani yamekuwa yakiandaa maandamano katika barabara za Burundi wakimshiniza rais huyo achie ngazi.
Makundi ya kuteteza haki za kibinafsi yanasema kuwa hadi kufikia sasa watu 70 wameaga dunia katika makabiliano baina ya polisi wa kupambana na fujo na waandamanaji.
Zaidi ya watu wengine 500 wamejeruhiwa katika kipindi hicho cha miezi miwili iliyopita.

null
Zaidi ya watu laki moja wametoroka nchini humo wakihofia fujo

Aidha zaidi ya watu laki moja wametorokea mataifa jirani kuepuka makabiliano na wengine kwa sababu ya hofu.
Mwezi uliopita jaribio la kumpindua madarakani bwana Nkurunziza lilitibuka.
Rais aliahirisha uchaguzi mkuu hadi tarehe 15 julai kufuatia shinikizo la viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Umoja wa mataifa unaendelea na jitihada za kuleta uwiano baina ya serikali na makundi ya upinzani.
Burundi imesema itafanya mazungumzo na wapinzani baada ya uchaguzi wa wabunge na madiwani, utakaofanyika Jumatatu ijayo.
Taarifa hii imekuja baada ya serikali kususia mazungumzo ya amani kati yake na wapinzani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa, na kusisitiza kuwa uchaguzi utafanyika licha ya wapinzani na shinikizo la kimataifa.
NA BBC SWAHILI
Makamu wa rais Burundi atoroka Makamu wa rais Burundi atoroka Reviewed by habari motto on 2:31 PM Rating: 5

Watu 7 Wafariki Baada Ya Kunywa Pombe Ya Kienyeji

8:14 AM

Hii sio mara ya kwanza kupata stori kutoka Kenya kuhusu pombe ya kienyeji kuua watu, imeingia kwenye headlines tena leo June 24 2015 ambapo watu saba wamefariki na wengine wamelazwa Hospitali baada ya kunywa na pombe ya kienyeji.

Baada ya kunywa pombe hiyo walianza kutetemeka na wengine wakashindwa kutembea, hii ikafanya watu wa Usalama kuingia mtaa mmoja baada ya mwingine katika Kaunti ya Kiambu, Kenya.

“Macho yalianza kuuma, nikaanza kuumwa na tumbo” >>> aliongea mmoja watu waliokunywa Pombe hiyo na kuzidiwa.

Mtu mwingine nae anasimulia; “Nilivyokunywa nilijisikia tu ulevi wa kawaida, baadae usiku nikajisikia kutetemeka”

Watu hao walikutwa wakiwa na hali mbaya pembeni ya barabara

Watu 7 Wafariki Baada Ya Kunywa Pombe Ya Kienyeji Watu 7 Wafariki Baada Ya Kunywa Pombe Ya Kienyeji Reviewed by habari motto on 8:14 AM Rating: 5

Marufuku ya biashara ya miraa,Kenya

7:52 AM
Ni mwaka mmoja tangu serikali ya Uingereza kupiga marufuku uuzaji na utumiaji wa miraa ama Mirungi nchini humo. Hatua ambayo ilipokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wadau wa zao hilo nchini Kenya.
Robert Kiptoo yuko mjini Meru, mashariki mwa Kenya eneo ambalo ndio linaongoza kwa ukulima wa miraa.Amewatembelea wakulima wa eneo hilo kuona wameathirika kiasi gani na hatua hiyo?

Marufuku ya biashara ya miraa,Kenya Marufuku ya biashara ya miraa,Kenya Reviewed by habari motto on 7:52 AM Rating: 5

Serikali ya Burundi Yaanzisha Operesheni Kabambe

7:47 AM
Serikali ya Burundi inaonyesha operesheni ya upunguzaji wa silaha kwa vijana wanachama wa vyama vya siasa waliokabidhiwa Silaha
"Sasa wakati umefika kurejesha silaha kwa wale ambao umiliki silaha kinyume cha sheria! "Hiyo ilikuwa onyo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumatatu, Juni 8, 2015, wakati wa mkutano kati ya CENI na washirika katika mchakato wa uchaguzi. Yeye, hata hivyo, alisema kuwa upunguzaji wa silaha utafanyika ndani ya wiki mbili, ili kuheshimu mapendekezo ya mkutano wa kilele mjini Dar-Es-Salaam.
Siku mbili kabla ya mwisho wa operesheni hii, maafisa wa Tume ambao wanausika kwa  operesheni hio awakutoa maelezo yoyote"Kazi inaendelea kwa upunguzaji wa silaha  na utakamilika baada ya wiki mbili,bado hatuna jibu ya kutoa mbele ya taifa kabla atuja maliza operesheni," alisema mtendaji wa tume waupunguzaji wa silaha.

Philippe Nzobonariba amesema kwamba serikali ya Burundi lazima iwe tayari kufanya kazi na waangaliziwa haki za binadamu na wataalam wa kijeshi, ili wapate ufumbuzi muzuri kwa upunguzaji wa silaha kwa vijana.
Hata hivyo, Alain Nyamitwe Aimé, Waziri wa Mahusiano ya Njeameweka masharti"Tunahitaji bayanakujuwa nchi gani ambayo itakuja na wataalam wa kijeshi, idadi yao, wapewe  mamlaka ya wazi. Kila kitu hutegemea juu ya kasi ambayo Umoja wa Afrika itachukua kwa  kesi hii. "
Upunguzaji wa silaha inatishia vitongoji ambazo zinapinga muula wa tatu wa raisi na waandamanaji."Maafisa wa polisi wanajifanya  kutafuta silaha, wakati katika hali halisi wanataka kutuzuia," anasemamkazi wa Kinanira.
Alhamisi iliyopita, alisema, wa polisi walitaka kutuweka chini ya ulinzi kwa sababu walikuta chupa tupu yaHeineken chumbani kwetu, lakini tumewaziwiya. "wametutumu kama tunatumia chupa izi kwa kutengeneza pombe bandiya" Mutakura vijana Anaongeza kuwa polisi walifika kuangalia silaha barabara ya  13Cibitoke,  walijaribu kuzuia kijana ila wakashindwa" walimtuhumu kuwa kijana uyo amewapiga mawe. "
Watu wanauliza kwanini operesheni hii inalenga vitongoji.vijana wa chama tawala CNDD-FDD awana wasiwasi wakati wao ndio wanao miliki silaha.
Leonce Ngendakumana anaamini kwamba upunguzaji wa silaha si kesi ya Waziri wa Mambo ya Ndani. Ili pawe upunguzaji wa silaha halisi, rais wa ADC-Ikibiri amesema kwamba wadau wote waje pamoja ili kufanya uchunguzi kwanza kisha Rais atachukua uamuzi wa sera juu ya kuwanyang'anya silaha na kupigwa mrufuku wa wanamgambo wake. "
anaamini kwamba mchakato huu lazima uwe wazi kwa sababu nikwa usalama wa nchi.
 Leonce Ngendakumana inaonyesha kwamba hii operesheni lazima wataalam wa kigeni ndio waje kuendesha kazi hii kwa usalama wa kila mtu.
"Serikali ambayo inawapa  silaha wanamgambo Imbonerakure hawezi kuwanyanganya. "anajuwa kwamba vijana hawo wana kazi ya kutetea muula wa Pierre Nkurunziza dhidi ya raia, hasa wa upinzani na vyama vya kiraia.
Leonce Ngendakumana
 Rais wa APRODH anasema kuwa chama kinachotawala  inawagawiya wa Imbonerakure silaha wakatiwengine wanataka kurejesha silaha. Ameongeza akisema : "Je, operesheni iyo wataweza  kwa wiki mbilitu wakati awakufaulu kwa zaidi ya miaka mitano"
Kwa M.Mbonimpa, suala la upungufu wa silaha sio kazi wala suala la polisi kwa sababu ni mapendekezo ya kila mtu. "Ni tume ya wataalam wa kigeni kusalimisha silaha kwa makundi yote ya vijana nawanachama wa vyama vya siasa wanaweza kuwahakikishia Burundi yote. "


Insurance                                Loans                                    Mortgage
GARI MPYAA... KWA BEI POA SANAA, NI RAHISI  SANA  KUIPATA>>>>  

Serikali ya Burundi Yaanzisha Operesheni Kabambe Serikali ya Burundi Yaanzisha Operesheni Kabambe Reviewed by habari motto on 7:47 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.