Diamond: Next stop NIGERIA #GloCAF_AWARDS

Baada ya kuujaza uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda na kuwapagawisha watoto wa Kagame siku ya Mwaka mpya, star wa Bongo, Diamond Platnumz anatarajia kutua kwenye ardhi ya kina Davido na Wizkid wiki ijayo.d n zDiamond ameweka wazi ratiba yake ya show zinazokuja ikiwemo moja ya Nigeria kwenye tuzo za ‘2014 Glo-CAF Awards’.
“Thank you KIGALI / RWANDA Next stop NIGERIA #GloCAF_AWARDS” aliandika kwenye post moja, “Thanks for the Mad Love RWANDA…i realy Appreciate it, Jus want you to know that Your Platnumz love you More… Next Stop! NIGERIA / DAR / ZANZIBAR / MWANZA / na “DIAMONDS ARE FOREVER” in DAR ES SALAAM!!!!” aliandika kwenye post nyingine.
Glo-CAF Awards ni tuzo za michezo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinazotarajiwa kutolewa Alhamisi ya Jan 8, 2015 huko Lagos, Nigeria.
Diamond: Next stop NIGERIA #GloCAF_AWARDS Diamond: Next stop NIGERIA #GloCAF_AWARDS Reviewed by habari motto on 11:55 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.