Mancity Yafika kileleni Ligi ya EPL

Manchester City yafika katika kilele cha uongozi wa ligi ya EPLbaada ya kuishinda Sunderland 3-2
Mchezaji Frank Lampard alifunga bao la ushindi kupitia kichwa chake dhidi ya Sunderland na kuiweka Manchester City sawa na Chelsea katika kilele cha ligi ya Uingereza.

Mabao ya Yaya Toure na Steven Jovetic yaliifanya Manchester City kudhibiti mechi hiyo.

Lakini timu hiyo ya nyumbani ilipoteza uongozi huo wa mabao mawili kwa mechi ya pili mfulululizo kupitia mabao ya Jack Rodwell na penalti ya Adam Johnson iliosawazisha.
Mchezaji Frank Lampard aliyeifungia Manchester City bao la ushindi.
Lampard alifunga bao la ushindi kupitia kichwa kizuri baada ya kupata krosi kutoka kwa Gael Clichy.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea ambaye atasalia katika timu hiyo baada ya Mancity kumuongezea mkataba hadi mwisho wa msimu kutoka New York City nusra afunge mabao matatu katika dakika 20 alizokuwa uwanjani ambapo City ilimaliza mechi hiyo kwa kishindo.

Source: BBC
Mancity Yafika kileleni Ligi ya EPL Mancity Yafika kileleni Ligi ya EPL Reviewed by habari motto on 4:23 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.