Breaking News: Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba Afariki Dunia

Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni. Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam. "Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry Komba mtoto wa marehemu. 

Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta. Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.

ripkomba
Breaking News: Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba Afariki Dunia Breaking News: Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba Afariki Dunia Reviewed by habari motto on 6:27 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.