MASTAA WA KIKE BONGO WANAISHI KWA KUUZA MIILI YAO?



Msanii wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda ‘Bella’.

IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya mastaa wa kike Bongo Muvi wanaishi kwa kuuza miili
 yao.
Akizungumza na waandishi wetu, msanii wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda ‘Bella’, 
alisema wasanii wengi wanaishi maisha ya thamani wakati kiuhalisia kazi yao haiwaingizii 
kipato kinachofanana na maisha ya thamani wanayoishi hivyo kuamua kujiuza.



“Filamu hazilipi, wengi tunajiuza. Bajeti yenyewe ya muvi ni ndogo, wasanii wengi wanataka 
kulipwa katika muvi moja, haiwezekani kumiliki vitu vya thamani ndiyo maana tunaamua
 kujiuza.
“Hakuna msanii anayeishi maisha ya kutegemea filamu, kwanza hazilipi kivile kama ambavyo
 wengi wanavyosema, ukweli ni kwamba wasanii tunajiuza ili tupate pesa ndiyo ituweke mjini
 tuendelee kung’aa,” alisema Bella.

Wakizungumza na waandishi wetu kwa masharti ya kutotajwa majina yao walikiri kuwa 
wasanii wengi wanajiuza kutokana na kutaka kuendana na hadhi ya umaarufu.



Mwigizaji Halima Yahya ‘Davina’. 


“Ukweli ndiyo huo, hakuna anayeweza kuishi maisha ya kumiliki magari ya kifahari, nyumba
 kwa kazi ya sanaa ni uongo mtupu,” alisema mmoja wa wasanii hao.

Alipoulizwa kuhusiana na ishu ya kujiuza, mwigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ alisema: 
“Binafsi naishi maisha ya kawaida, najua wapo wanaojiuza, nawapa pole maana wanapenda 
maisha ya mteremko, mimi siyaungi mkono kabisa.”

Alipotafutwa mwigizaji Halima Yahya ‘Davina’ naye alikiri: “Wasanii wengi Bongo 
wanategemea kuhongwa na mabwana tofauti ili wapate jeuri ya kujifanya wanazo, utakuta 
anatengeneza nywele za milioni mbili au kanunua nguo ya milioni kumi huo ni uongo tu, 
filamu hazilipi kiivyo wengi wanataka kuiga maisha ya wasanii wa nje.”

Chanzo:global publishers
MASTAA WA KIKE BONGO WANAISHI KWA KUUZA MIILI YAO? MASTAA WA KIKE BONGO WANAISHI KWA KUUZA MIILI YAO? Reviewed by habari motto on 7:11 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.