Wananchi Wamkaanga Mkuu Wa Kituo Cha Polisi Anayewanyanyaa

Wananchi mbalimbali wanaishi Kinondoni Moscow Kata ya Hananasif wamemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Mathias Chikawe kumuondoa Mkuu wa kituo Kidogo cha Polisi cha Hananasif aliyefahamika kwa jina la SajentDeogratus kwa madai ya kuwanyanyasa kwa kauri mbaya na kuwafokea bila kuwapatia huduma. Wakiongea na gazeti moja hivi karibuni wananchi walisema kuwa mkuu huyo wa kituo ambae ni mtu mzima amepelekea Wananchi kuanza kulichukia Jeshi hilo kupitia yeye kwa vile ameshindwa kuwa na ushirikiano nao hali inayoondoa amani katika kitongoji hicho. Aidha wakazi hao walimaliza kusema wana imani na wakuu wa idara hiyo kwani licha ya Serikali za mtaa huo kuitia Mwenyekiti wao Selemani Rada kupeleka taarifa kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa ajiri ya kubadilishiwa mkuu huyo wa kituo lakini imekuwa patupu. Wananchi

walimaliza kusema kuwa kutokana na mtaa wao kuhitaji mkuu wa kituo mwenye kichwa ngumu na mchapakazi wameliomba Jeshi hilo kumrejesha aliyewahi kuwa mkuu wa kituo hicho Sajent Chalo ambae aliweza kusambaratisha uharifu wote kiasi cha vijana wengi kustaafa uharifu na kujiingiza kwenye vikundi vya biashara ili kujipatia pesa kwa njia harali. Aisha Sajent Chalo pia alikuwa na mbinu za kisasa za kuondoa uharifu ni pamoja na kukaa vikao mara kwa mara na vijana hao wa kihuni na kuwasihi kaucha uharifu hali iliyozaa matunda na sasa wamemuomba Kamanda Wambura kufanya jitihada za kumrejesha Sajent Chalo haraka ili kunusuru hali ya usalama katika eneo hilo.
Wananchi Wamkaanga Mkuu Wa Kituo Cha Polisi Anayewanyanyaa Wananchi Wamkaanga Mkuu Wa Kituo Cha Polisi Anayewanyanyaa Reviewed by habari motto on 6:51 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.