Auawa NaKunyofolewa Nyeti Zake

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 09.03.2015.

·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA UTURO WILAYANI MBARALI AMEKUTWA AMEUAWA NA KISHA KUNYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI.

·         MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MOMBA.

·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA WAKIWA NA POMBE YA MOSHI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MKAZI WA UTURO WILAYANI MBARALI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LACHARLES SIJAONA @ MATEMLA (55) ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA SHINGONI. AIDHA MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA UMENYOFOLEWA SEHEMU ZA SIRI NA WATU HAO.

MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NJE YA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI MNAMOTAREHE 08.03.2015 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTURO, KATA YA MAPOGOLO, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.

CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISINYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA MSAKO/UPELELEZI WA KUWABAINI WALIHUSIKA KATIKA TUKIO HILI UNAENDELEA.



KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA KATIKA SHULE YA MSINGI CHIPAKA ILIYOPO WILYANI MOMBA KATIKA KIJIJI CHA NKANGAMO ALIYETAMBULIKA KWA JINA LAENES DADISON (08) ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI  T.288 BCH AINA YA TOYOTA CRESTA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.03.2015 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONIHUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA NKANGAMO, TARAFA YA TUNDUMA, KATIKA BARABARA YA TUNDUMA/SUMBAWANGA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. 

CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. AIDHA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA SERIKALI TUNDUMA. 

TAARIFA ZA MISAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ESTER MWAKALINDILE (33) MKAZI WA NDOLA 2. AYUBU MWANZYELE (28) MKAZI WA MAPELELE 3. JOHN EMMANUEL (40) MKAZI WA NDOLA 4. SAMWEL MWAKALINGA (30) MKAZI WA NDOLA 5. ISSAMBI MWALYEGO (48) MKAZI WA DDC 6. WEMA AMBAKISYE (32) MKAZI WA NDOLA NA 7. ANGOLUISYE MWAMBAPA (26) MKAZI WA NDOLA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 08.03.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO MAENEO YA NDOLA KILABUNI, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISINYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA KUFANIKISHA KUKAMATWA KWA DEREVA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO AJALI AZITOE KWA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

                                             
                                                     Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Auawa NaKunyofolewa Nyeti Zake Auawa NaKunyofolewa Nyeti Zake Reviewed by habari motto on 4:39 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.