Manchester United Wataka kumrudisha Ronaldo

kiatuKlabu ya Manchester United imeanza mazungumzo na wakala wa  mchezaji Christiano Ronaldo anayeichezea Madrid kwa lengo la kumrudisha katika klabu yake hiyo ya zamani ya Old Trafford.
Kumekuwa na uvumi kuwa mchezaji huyo haridhishwi na maisha anayoishi katika klabu yake ya sasa ya Real Madrid na huenda safari yake ya kurudi Manchester United ikiwa kweli baada ya viongozi wa timu hiyo kuanza mazungunzo na bosi wake Jorge Mendes.
Kwa mujibu wa gazeti la Metro la Uingereza, United ina matumaini ya kumpata Ronaldo kwa kitita cha Euro millioni 100 ambazo ni sawa na pauni millioni 71.1.
Uhakika wa raia huyo wa Ureno kukubali kurudi Manchester United upo juu yake, licha ya kuipenda klabu hiyo.
Insurance  
Manchester United Wataka kumrudisha Ronaldo Manchester United Wataka  kumrudisha Ronaldo Reviewed by habari motto on 2:32 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.