Ajali Nyingie Yaua Mikumi

WATU wawili wamekufa papo hapo na wengine 48 kujeruhiwa na baadhi yao 12 kulazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito  ya Mikumi kufuatia  basi lenye namba za usajili T 618 BDN aina ya Scania la Happy Nation likitokea Dar es Salaam kwenda  Mkoani Mbeya kupinduka eneo la Mikumi ,wilayani Kilosa ,mkoa wa Morogoro kwenye barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alithibitisha leo kutokea kwa ajali hiyo  majira ya mchana na kupoteza  uhai wa watu wawili ambao mwanaume mmoja na mwingine ni mwanamke na pia kujeruhi wengine 48  katika eneo la ndani ya hifadhi ya taifa ya Mikumi , barabara kuu ya Morogoro- Iringa.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo ambaye alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake,  bila kuchukua tahadhari na alipoona kuna gari jingine likija kutoka upande wa Iringa aliamua kutanua  upande wake zaidi na kujikuta likiacha njia na kupindula mara tatu .
Hata hivyo alisema baada ya kutokea kwa ajali hiyo , dereva wa basi alikimbia eneo hilo na anatafutwa na Polisi, ambapo majeruhi hao 48 , kati yao 12 wakiwemo wanawake sita na wanaume sita wamelazwa  katika hospitali ya Misheni ya St Kizito ya Mikumi na wanaendelea vizuri.
Ajali Nyingie Yaua Mikumi Ajali Nyingie Yaua Mikumi Reviewed by habari motto on 9:17 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.