Kesi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja Yapigwa Kalenda Hadi Mei 7 Mwaka Huu


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja leo amefikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ya kesi inayomkabili ya uchochezi, lakini upande wa serikali ulikuwa haujakamilisha kuandika maelezo hayo.
 
Mwendesha mashtaka mwandamizi wa serikali, Rose Shio aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilifika mahakamani hapo leo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali lakini upande wa serikali ulikuwa bado haujakamilisha kuandika maelezo hayo ya awali.
 
Amesema kuwa kesi hiyo leo imekuja mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa awali lakini kwa bahati mbaya upande wa serikali umeshindwa kuandika maelezo ya awali kwa hiyo akaomba ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya awali ya kesi hiyo.
 
Wakili wa mshtakiwa huyo Godfrey Wasonga amesema hana kipingamizi na ombi hilo la mwendesha mashtaka wa serikali na kuomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
 
Baada ya maelezo hayo, hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Rhoda Ngimilanga alisema kesi hiyo itatajwa tena Mei 7 mwaka huu na mshtakiwa ameendelea kuwa nje kwa dhamana.
Kesi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja Yapigwa Kalenda Hadi Mei 7 Mwaka Huu Kesi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja Yapigwa Kalenda Hadi Mei 7 Mwaka Huu Reviewed by habari motto on 10:27 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.