Kama kuna kitu kinasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mchezo wa soka duniani, basi ni mchezo wa mahasimu wa jadi wa jiji la Manchester – matajiri wa Manchester City dhidi ya Manchester United.![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_uTGZB18ji4G74QGxymZkt7g2_D6UIfR50QQNZklZ4QeQwrW1ZCY_BjeNcKUZ33qghk5xwspDrZb-jtHruXrfZlzRtH9eq5NwgeT0J74QOUb3Za5QNA_3yiGfW0ZwPk1vdO_NcNz_Oondy3ec9qtrsRDzw2GXL0VqeeWzfV2Q=s0-d)
Kwa miaka mingi rangi nyekundu imekuwa ikitawala jiji hilo, lakini lakini katika kipindi cha miezi 16 iliyopita hali imekuwa tofauti – rangi ya blue imekuwa ikitawala jiji hilo.
Hata hivyo kwa mara ya kwanza tangu November 23, 2013 – Manchester United wataikaribisha City, Old Trafford, wakiwa wapo juu ya Manchester City kwenye msimamo wa ligi kuu ya England – wakiwa wamecheza idadi sawa ya mechi.
Mara ya mwisho kwa Man United kuwa juu ya City kwenye msimamo wa ligi – ilikuwa baada ya mechi 11 katika msimu wa 2013/14 – wakiwa chini ya Sir Alex Ferguson – United walikuwa mbele ya City kwa pointi 1 kwenye msimamo.
Jumapili hii timu hizo zinakutana katika dimba la Old Trafford huku Manchester United wakiwa mbele kwenye msimamo wa kwa pointi 62, na wapinzani wao City wakiwa na pointi 61.
Huenda ulikuwa hujui ni lini mara ya mwisho Man Utd kuwa juu ya City kwenye EPL – hii hapa
Reviewed by habari motto
on
12:20 AM
Rating: