Wasanii ambao waliwahi kuwa wapenzi
rapper Isaack Waziri “Lord Eyez” Makuto na muimbaji Rehema “Ray C”
Chalamila hivi karibuni watasikika kwenye ngoma waliyofanya pamoja
Lord Eyez ameiambia Clouds Fm kuwa wimbo huo ambao amemshirikisha
ex-wake Ray C unaitwa ‘Matatizo’ umefanywa kwenye studio ya Mandugu
Digital chini ya producer aitwaye Shaqee.
“Ngoma imeelezea mambo mengi kuhusu maisha kama jina linavyojieleza
imeshakamilika kila kitu nitaitambulisha hivi karibuni kwenye kipindi
cha xxl,”alisema Lord Eyez.
Mwaka jana (2014) Ray C alionesha nia ya kutaka kumsaidia Lord Eyez
kwa kumshauri abadili mwenendo wa maisha yake na aachane na matumizi ya
dawa za kulevya yaliyokuwa yakimsababisha rapper huyo kuingia kwenye
majanga kila mara, pia alimkaribisha kutumia tiba ya Methadone
Lord Eyez Na Ray C Pamoja Tena ‘Soon’.
Reviewed by habari motto
on
9:38 PM
Rating:
