Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
‘Nandwa alitimuliwa na uongozi wa Coastal muda mfupi baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC Machi 22 mwaka huu ingawa baadaye ilielezwa kuwa aliamua kuondoka mwenyewe kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo ligi kuu.’
UKIMUONA wa nini, wenzako wanasema watampata lini. Msemo huu
umejidhihirisha baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Coastal Union FC,
Mkenya James Nandwa, kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa Shabana FC.‘Nandwa alitimuliwa na uongozi wa Coastal muda mfupi baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC Machi 22 mwaka huu ingawa baadaye ilielezwa kuwa aliamua kuondoka mwenyewe kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo ligi kuu.’
Katika muda wake wa siku chache na timu hiyo ya Kisii, Kenya, Nandwa amebainisha kuna tatizo la kukosekana kwa umoja ndani ya klabu hiyo ya nchini mwake.
Pia amebainisha kuwa safu ya umaliziaji ya kikosi hicho ni dhaifu kiasi cha kutokuwa na madhara kwa timu pinzani.
“Tatizo kubwa la Shabana ni safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa ikishinda kuzitumia nafasi inazozipata. Tutalifanyia kazi suala hili ili tufanye vizuri,” Nandwa amekaririwa na moja ya mitandao ya michezo ya Kenya.
Kocha aliyetimuliwa Coastal apata timu Kenya.
Reviewed by habari motto
on
9:34 PM
Rating: