Mbeya City Motto Wa Kuotea Mbali Msimu Ujao

Mbunge wa Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi
amewataka mashabiki wa
Mbeya City kutokata
tamaa kutokana na
mwenendo wa timu yao
msimu huu.
Mbilinyi maarufu kama
Sugu amesema upepo
mbaya umepita Mbeya
City msimu huu na ana
imani kikosi kitafanya
vema zaidi.
“Mimi ndiyo mbunge
wao, Mbeya City, najua
watu wana mapenzi
makubwa na timu yao.
Viongozi nao
wanapambana.
“Mimi ni shabiki
mkubwa, ndiyo maana
nina imani mambo
yatakwenda vizuri
msimu ujao.
“Wana Mbeya wanapaswa
kusaidiana pia kuwa
wavumilivu katika
kipindi hiki,”
alisema.
Pia Sugu alitoa
shukurani kwa
wadhamini wao Bin Slum
Tyres Ltd kutokana na
udhamini wao.
“Ni watu wanaotakiwa
kupewa shukurani,
wameiamini Mbeya na
Wanambeya wanaijua
dhamani yao.
“Tunaamini tutaendelea
kuwa nao, lengo ni
kuisaidia timu hiyo ya
Wanambeya,” alisema.
Kampuni ya Bin Slum
ndiyo wadhamini wakuu
wa Mbeya City kupitia
betri zao za RB.
Mbeya City ilifanya
vema msimu uliopita,
lakini ikashindwa
kurejea msimu na
mwendo wake kuwa wa
kusuasua.

Mbeya City Motto Wa Kuotea Mbali Msimu Ujao Mbeya City Motto  Wa Kuotea Mbali Msimu Ujao Reviewed by habari motto on 4:16 PM Rating: 5
Powered by Blogger.