Kutoka Burundi;Baada ya Jaribio La Mapinduzi

Burundi kwa sasa ndiyo nchi inayozungumzia sana kutokana na vita ya kisiasa inayoendelea tangu Rais wakePierre Nkurunziza atangaze uamuzi wake wa kutaka kuwania Urais kwa awamu ya tatu mfululizo.

Jaribio la kutaka kumpindua madarakani wakati akiwa Tanzania kwenye mkutano wa usuluhishi pamoja na Marais wengine wanaounga Jumuiya ya Afrika Mashariki, halikufanikiwa na sasa uamuzi uliofikiwa ni kuahirishwa kwa uchaguzi wa Wabunge ili kuzunguzia mustakabali mzima unaoendelea nchini humo.

Stori mpya iliyotufikia leo ni kwamba pamoja na machafuko yanayoendelea nchini humo Rais huyo ameonekana kutojali na kuna picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao zikimuonyesha akiwa uwanjani na wenzake akicheza mpira huku akionekana mwenye furaha

Imeelezwa kuwa leo mtu mmoja amepigwa risasi ya mgongoni na askari wanaolinda usalama katika mji wa Bujumbura wakati wakiandamana.

Kutoka Burundi;Baada ya Jaribio La Mapinduzi Kutoka Burundi;Baada ya Jaribio La Mapinduzi Reviewed by habari motto on 6:22 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.