Simba Kumnasa Kiungo Toka Burundi

Wakongwe Simba wana tatizo katika safu yake ya ushambuliaji. Sasa wameanza harakati za kusajili straika wa maana ili aifungie mabao msimu ujao na sasa ipo katika mazungumzo na mshambuliaji wa Kiyovu SC ya Rwanda, Laudit Mavugo
raia wa Burundi.
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ndiye
aliyepeleka jina la Mavugo kwa Kamati ya
Usajili ya timu hiyo ili asajiliwe baada ya Dan
Sserunkuma kuondoka kikosini.
Mmoja wa mabosi wa kamati ya usajili amesema, Mavugo anaelezwa kuwa
na uwezo unaofanana na Amissi Tambwe wa Yanga ambaye pia ni raia wa
Burundi kama yeye. Alisema tayari Kopunonic ambaye hatma yake ipo
shakani Simba, ameshawasiliana mara
kadhaa na Mavugo mwenye umri wa miaka 25 ili aje kumaliza tatizo la ufungaji mabao klabuni hapo.
“Kuna straika alianza mazungumzo na uongozi baada ya Kopunovic kuweka wazi sifa zake, anatokea Burundi na aliwahi
kufanya kazi katika timu ya Polisi ya Rwanda,” alisema.
Mavugo aliyewahi kuichezea Vital’O ya
Burundi alilazimika kuondoka Polisi ya Rwanda baada ya kuibuka kwa
sheria mpya ya kupunguza idadi ya wachezaji wageni. Hata hivyo
kusajiliwa kwake Simba kutategemea na uwepo wa Kopunovic kikosini.

Simba Kumnasa Kiungo Toka Burundi Simba Kumnasa Kiungo Toka Burundi Reviewed by habari motto on 6:38 PM Rating: 5
Powered by Blogger.