
Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, Jamal Kisongo amesema hatma ya mshambuliaji huyo kucheza soka la kulipwa Ulaya sasa itasubiri mwakani kutokana na rais na mmiliki wa klabu yake yake TP Mazembe Moise Katumbi kuonesha bado anahitaji huduma yamchezaji huyo hususan katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika.
“Katumbi ameonesha bado anahitaji kumtumia katika kikosi chake kwenye michuano ya champions league kwa maana hiyo makusudio yetu na matarajio yetu, kunatimu moja kubwa ilitaka kumsaini kwa ‘Euro’ milioni moja lakini bahati mbaya Katumbi alitaka amuache baada ya champions league kuisha”, amesema wakala huyo wa Samatta.
HII NDIO HATMA YA SAMATTA KUCHEZA SOKA ULAYA…
Reviewed by habari motto
on
4:40 PM
Rating:
