Rais Paul Kagame wa Rwanda amezikosoa nchi za Magharibi kwa hatua ya kumtia mbaroni Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya nchi yake huko Uingereza.
Rais Kagame ameelezea ukosoaji wake huo katika hotuba aliyoitoa mbele ya Bunge la Rwanda hii leo na kusema kuwa, kitendo cha kumtia mbaroni Jenerali Karenzi Karake, Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya nchi hiyo kuwa ni cha kulidhalilisha taifa lake.
Rais Kagame amesema kuwa, huwenda maafisa wa Uingereza walimfananisha Jenerali Karake na wahajiri haramu na ndio maana wakamtia mbaroni na kusisitiza kuwa, Wamagharibi wanamchukulia kila mtu mweusi kuwa ni mhajiri haramu.
Amesisitiza kuwa, siku zote watu weusi katika nchi za Kimagharibi wanakumbwa na ukandamizaji na ukatili kutokana na wao kuwa weusi.
Karenzi Karake mwenye umri wa miaka 54 alifikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya Westminster baada ya kukamatwa kufuatia waranti uliotolewa na jaji wa mahakama ya Uhispania, Fernando Andreu, kwa madai ya kuhusika katika jinai za kivita dhidi ya raia.
Kutiwa mbaroni Karake kumeibua hasira kali kwa serikali ya Rwanda. Kwa mujibu wa serikali ya Kigali, kutiwa mbaroni afisa huyo wa usalama kumefanyika kwa sababu za kisiasa.
Chanzo kiswahili.irib.ir
Rais Kagame ayakosoa vikali madola ya Magharibi
Reviewed by habari motto
on
9:26 AM
Rating: