![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTIaeoPznVoP252hxDPq7Zbn3q3Yl8YFpLueoGZO_PgHYfYNj5voviekTCPJrOM8nneiVjZ22dSs_z0_AhyOvUvJ0L7NeKXU-odivThP2WLbEycIOEAuM5F5vkbpVcyOsuOTm1Yzwrtn0k/s1600/1-Osine-and-Anesi.jpg)
Vijana wawili wadogo wa Nigeria,Osine Ikhianosime miaka 13 na kaka yake Anesi Ikhianosime miaka 15 walishangaza dunia kwa kugundua Application ya kutumika kwenye simu za kisasa maarufu kama smartphone unaojulikana kama
‘Crocodile Browser Lite'.Vijana hao ambao kiukweli wameleta changamoto kubwa kwenye maswala ya teknolojia waliweza kufanya kazi hii kwenye muda wao ambao wanakuwa hawana shughuli ya kufanya.Wanadai kwamba walichoshwa sana na Application inayotumika sana kwa sasa ambayo ni Google Chrome.Osine anaendelea kusema kuwa yeye aliandika code na kaka yake akatengeneza muundo mzima wa Application hiyo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhUduVz4ZXIQJ8cRQj2Ni3yws8G7yfVzn1v0NZo5qJe_BRcH5OgeGZ0umkOP5QcL-mcYBNEhHkwcYmOo3zx5IkK7-ttFiey100JQJQ-LqrIXtaydgS9GG2FWEAK0YbDbHXgli8nPy4zBNnp/s1600/crocodile-browser-lite-founders.png)
Osine ambaye alizaliwa Aprili 28, 2001 alianza kupenda mifumo ya kompyuta akiwa na umri wa miaka saba wakati huo kaka yake ana miaka tisa.Kipindi hicho ndio walikuja na wazo la kuanzisha kampuni.Mwanzo kabisa waliita software hiyo Door kutokana na Microsoft kuita yake Window lakini wakagundua kwamba tayari imeshatumika ikawalazimu kubadilisha jina na kuwa BluWindows.
Insurance Loans Mortgage
BONYZA HAPA CHINI KUONA VIDEO ZOTE MPYA ZA WASANII WA TANZANIA
Vijana wa Nigeria waapa kula sahani moja na Bill Gates
Reviewed by habari motto
on
7:56 AM
Rating:
![Vijana wa Nigeria waapa kula sahani moja na Bill Gates](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTIaeoPznVoP252hxDPq7Zbn3q3Yl8YFpLueoGZO_PgHYfYNj5voviekTCPJrOM8nneiVjZ22dSs_z0_AhyOvUvJ0L7NeKXU-odivThP2WLbEycIOEAuM5F5vkbpVcyOsuOTm1Yzwrtn0k/s72-c/1-Osine-and-Anesi.jpg)