Sentensi 57 za Maneno Mazito Aliyozungumza DK SLAA Hizi Hapa.

Waandishi wa Habari Dar es salaam na kuzungumza mambo mbalimbali yaliyomfanya kuwa kimya ndani ya Chama chake cha CHADEMA.

Hapa nimekuwekea  maneno aliyokuwa akiyazungumza mbele ya vyombo mbalimbali vya Habari.

WILIBROD SLAA-Katika maisha yangu yote sijawahi kuona waandishi wengi hivi, ni dalili kwamba watu wanakiu ya kujua

WILIBROD SLAA-Ningependa nianze kwamba niliamua kufanya kazi hii leo kwa sababu inafika mahali ukweli lazima usemwe

WILIBROD SLAA- Wengi mnafahamu kwamba sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia kile ambacho ninakiamini mimi

WILIBROD SLAA-Niseme tu pia sina chuki na mtu yoyote wala kiongozi yoyote wa chama chochote ingawa nimesikia mengi

WLIBROD SLAA-Mimi sikuwa likizo kama mlivyoambiwa na wengine, kuna mambo ambayo yalinifanya niwe kimya kwa muda

WILIBROD SLAA-Niliamua kuachana na siasa baada ya kuona mambo hayaendi sawa kama nilivyotegemea ndani ya chama changu

WILIBROD SLAA-Baada ya LOWASSA kutajwa, mpambe wake Askofu GWAJIMA alinipigia simu akiniambia Dodoma mambo yameiva

WILIBROD SLAA-‘Kama utaratibu, LOWASSA baada ya kusema anahama CCM, alipaswa ajisafishe na tuhuma zote alizokuwa nazo

WILIBROD SLAA-LOWASSA hakufanya hivyo, alipaswa kufanya hivyo akiwa peke yake na si viongozi wa chama anachokwenda

WILIBROD SLAA-Si kwamba nilikuwa sitaki LOWASSA agombee Urais,nilitaka tupate mgombea mwenye sifa zote zinazotakiwa

WILIBROD SLAA-Mimi sikuwa na shida ya kugombea Urais, ningekuwa nataka ningechukua fomu siku ya kwanza walipotangaza

WILIBROD SLAA-‘Wakati hayo yanaendelea nilikuwa nasimamia uteuzi wa viongozi mbalimbali ndani ya CHADEMA

WILIBROD SLAA-Sikuambiwa lolote kama LOWASSA ni Asset au liability ndani ya Chama chetu na ndio maana nilikuwa sielewi

WILIBROD SLAA-‘Niliandika barua ya kujiuzulu lakini Prof SAFARI akaichana, sikukata tamaa nikaandika tena

WILIBROD SLAA-Niliandika tena taarifa rasmi kupeleka kwenye chama,hawajui ukitaka kujiuzulu haina hata haja ya kueleza

WILIBROD SLAA-Maneno mengi yalisemwa mara nimefungiwa ndani na mke wangu, mara nitaitisha kikao na waandishi kesho

WILIBROD SLAA- Walisema Dk Slaa analipwa milioni 7 na CHADEMA,napenda kusema familia yangu inaishi maisha ya kawaida

WILIBROD SLAA-Mimi na SUMAYE tunagombana kila siku kwa kuchukua shamba kubwa pale Kibaigwa, alafu leo anajiita msafi

WILIBROD SLAA-Niliahidi mwaka huu CHADEMA hatuchukui Makapi, lakini naona wote waliokuja ni mizigo, nawajua A mpaka Z

WILIBROD SLAA- Ndio maana mpaka leo viongozi wangu wamebaki vigugumizi ndio maana mpaka leo hawawezi kusema lolote

WILIBROD SLAA-‘Leo LOWASSA anasimama jukwaani na kusema leteni ushahidi wa ufisadi hata bado hajapewa kadi ya chama

WILIBROD SLAA-‘CCM wamekuwa waoga kutoa ushahidi wa mafisadi, na hata LOWASSA alipofikia ni CCM imemlea

WILIBROD SLAA-‘Mwaka 2008 Nilikuwa bungeni kuzungumzia Richmond, tuliyajadili Bungeni wote,hatukuyasoma magazetini

WILIBROD SLAA-‘Mimi ninamlaumu LOWASSA kwa mambo mengi sana na si kashfa ya Richmond pekee kama watu wanavyofikiria

WILIBROD SLAA-‘Ni bora nipotee kwenye siasa kabisa kuliko kukumbatia mambo maovu kama haya yanayoendelea sasa

WILIBROD SLAA-‘Ni bora nipotee kwenye siasa kabisa kuliko kukumbatia mambo maovu kama haya yanayoendelea sasa

WILIBROD SLAA-Mimi nimeletewa rushwa hadharani asubuhi, nikamwambia kama unanipa milioni 500 nyingine unazitoa wapi?

WILIBROD SLAA-‘Milioni 500 ni nyingi sana, Rushwa ni kitu kinachoanzia kichwani na si katika mazingira ya kawaida

WILIBROD SLAA-‘Mnaweza kusema kwa nini namsema LOWASSA tu, mkumbuke anagombea Urais wa nchi, ukweli hawezi kuvumilika

Dr.WILIBROD SLAA-‘Nilimwambia LOWASSA wewe na wenzako ni mafisadi kichwani, kwenye nafsi na moyoni alafu nikakimbia

Dr.WILBROD SLAA-Nimemsikia MWAKYEMBE na SITTA wanamuomba LOWASSA kwenye mjadala ili aweze kueleza mambo yake, safii

Dr.WILBROD SLAA-Nimemsikia MWAKYEMBE na SITTA wanamuomba LOWASSA kwenye mjadala ili aweze kueleza mambo yake, safii

WILBROD SLAA-‘Naumia sana kuona CHADEMA yangu niliyotoka nayo mbali na kufika hapa leo inafikia hatua haiaminiki tena

WILBROD SLAA-Sehemu kubwa ya hotuba ya Jangwani ni ilani yetu ambayo tulishaandika toka zamani,LOWASSA hakuweka kipya

Dr.WILIBROD SLAA-‘LOWASSA achunguzwe zaidi ya milioni 400 alizopeleka Marekani, wanaomtetea watoke hadharani wakitaka

Dr.WILBROD SLAA-‘Vijana wengi wakisikia CHADEMA wanashawishika, lakini napenda kuwaambia baadaye tusije kulaumiana

Dr.WILBROD SLAA-Mimi huwa naongea kwa kujiamini sana, na siwezi kwenda kushtaki mahakamani, anayetaka kwenda aende

Dr.WILBROD SLAA-‘Mimi sitaki kuingilia sana mambo ya Kina Babu Seya lakini naomba wanasheria wetu wajitokeze kusema

Dr.WILIBROD SLAA-‘Akili ya LOWASSA ipimwe,kesi ya ulawiti Rais hapaswi kuingilia, anaingilia uhuru wa mahakama

Dr.WILBROD SLAA- Afadhali kutokuwa na Rais kama huyo,ni Rais balaa ambaye hawezi kuthamini maisha ya Watanzania

Dr.WILBROD SLAA-‘Akiwa Waziri mkuu alibadilisha hata mpaka wa Monduli na Karatu ambapo mgogoro upo mpaka sasa

Dr.WILBROD SLAA-Nimestaafu siasa ina maana sina Chama lakini haimaanishi sina nchi, nitabaki kuwa mtetezi wa wanyonge

Dr. WILBROD SLAA-Nimeombwa kugombea Urais karibu vyama vitano nimekataa kwa kuwa siamini wala sitaki kuyumbishwa

DR.WILBROD SLAA-Najua hela za ROSTAM AZIZ ndio zinasaidia mambo ya uchaguzi, pesa zinagawanya kila kona ya nchi

Dr.WILBROD SLAA-‘Hakuna kipindi nimepata vitisho kama hiki, hata kipindi cha kutaja List of shame haikuwa hivi

Dr WILBROD SLAA- ‘Kama kuna Maaskofu mmehongwa nchi hii ni bora mkaenda mbele za Mungu kutubu na kuomba msamaha

Dr.WILBROD SLAA-Narudia tena siendi wala sitakwenda chama kingine chochote nitakuwa Mtanzania wa kawaida kama wengine

Dr WILBROAD SLAA-Namtaka LOWASSA leo atoke hadharani atuambie Richmond ni ya Nani? na huyo mkubwa ni nani? si kazi rahis

Dr WILBROD SLAA-‘Nataka ripoti ya Richmond iwekwe hadharani ili wale wanaopiga propaganda waadhirike ili watu wawaelewe

Dr WILBROAD SLAA-Sina sababu ya kurudisha kadi, ni sawa na kadi ya ndoa,ni mali yangu, ni kumbukumbu katika maisha yangu

Dr. WILBROD SLAA-Sina ugomvi na MBOWE ni vyema nikasema, hata nyumba ninayoishi alinisaidia, itakuaje niwe na chuki naye

Dr.WILBROD SLAA-CCM wanilitaka niachie jimbo la Karatu mwaka 2000, nikawaambia sharti saini 3, ya Rais, yangu na ya YESU

DR WILBROD SLAA- Nilimshukuru Mungu kutokwenda CCM kwa sababu ningefukuzwa ndani ya miezi mitatu kwa kuwa nisingekubali

DR WILBROD SLAA-Simpigii kampeni mtu yoyote lakini nimefanya utafiti kuona Taifa litapata hasara gani akichaguliwa LOWASSA

Dr WILBROD SLAA-Niliambiwa nina dk5 za kuishi, piga magoti muombe Mungu wako akusaidie baada ya kutaja ufisadi wao

Dr.WILBROD SLAA-‘Kuhama chama ni jambo la kawaida katika siasa, tatizo anayehama chama huko alipokuwa awali alikuwaje?

Dr.WILBROD SLAA-‘Kuhama chama ni jambo la kawaida katika siasa, tatizo anayehama chama huko alipokuwa awali alikuwaje?

Dr. WILBROD SLAA-‘Silaha huziweki zote mezani, nimewaomba wahusika wajitokeze, wakifanya hivyo nitarudi tena kuzungumza
-via millardayo

Sentensi 57 za Maneno Mazito Aliyozungumza DK SLAA Hizi Hapa. Sentensi 57 za Maneno Mazito Aliyozungumza DK SLAA Hizi Hapa. Reviewed by habari motto on 9:01 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.