Alpha Conde ametangazwa kuwa Rais wa Guinea, baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika jumapili iliyopita.
Ameshinda kwa asilimia 58 ya kura.
Tume ya uchaguzi ya Guinea, imetangaza matokeo haya ya uchaguzi ambayo sasa inamaanisha kuwa rais Conde ataanza rasmi muhula wake wa pili bila ya kuwa na marudio ya uchaguzi huo mkuu.
Hata hivyo matokeo hayo yamepingwa na viongozi wa upinzani.
Kinara mkuu wa upinzani Cellou Dalein Diallo, alijiondoa katika uchaguzi huo Jumatano iliyopita akidai kuwa ulikumbwa na udanganyifu.
Sasa ameitisha maandamano ya amani.
Wachunguzi wa kimataifa waliokuweko huko wanasema kuwa, kulikuwa na hitilafu hapa na pale siku ya upigaji kura, lakini haukuwa mkubwa kiasi cha kutatiza matokeo ya uchaguzi huo.
Alpha Conde atangazwa rais wa Guinea
Reviewed by habari motto
on
12:35 PM
Rating: