Kipigo kilichowakuta AS Roma kwa FC Barcelona bora ya Real Madrid, haya ndio matokeo ya mechi za UEFA Nov 24 (+Video)
Mshikemshike wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi imeendelea tena usiku wa November 24 katika viwanja mbalimbali barani Ulaya, usiku wa November 24 zimechezwa jumla ya mechi nane zinazohusisha timu kutoka Kundi E, F, G na H, miongoni mwa mechi zilizochezwa na kushuhudia idadi kubwa ya magoli ni mechi kati yaFC Barcelona dhidi ya Roma.
Huu ukiwa ndio mchezo wa pili wa Lionel Messi toka arejee dimbani baada ya kuuguza jeraha la goti kwa zaidi ya wiki tatu, Roma ambao walikuwa ugenini katika dimba la Nou Camp jijini Barcelona walipata bahati mbaya kurejea kwa nyota huyo wa kimataifa waArgentina, kwani alionekana kama mtu ambaye hajatoka majeruhi kutokana na kuendelea kucheza katika kiwango bora.
FC Barcelona walifanikiwa kuiadhibu Roma kwa jumla ya goli 6-1 magoli ambayo yalifungwa katika mfumo ule ule wa FC Barcelona uliyozoeleka wa pasi fupi fupi lakini zenye madhara kwa Roma. Ilichukua dakika 15 za mwanzo tu FC Barcelona kupata goli la kwanza baada ya Luis Surez kuitumia vyema pasi kutoka kwa Dani Alves.
Goli la pili la FC Barcelona lilifungwa na Lionel Messi dakika ya 18 ya mchezo kabla yaLuis Suarez kufunga goli la tatu dakika ya 44, goli la nne lilifungwa na Gerrard Piquedakika ya 56, Lionel Messi dakika ya 60 kabla ya Adriano kupachika goli la sita dakika ya 77, Roma ambao walikuwa hawaamini kilichowakuta walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi kutoka kwa Edin Dzeko dakika ya 90.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizochezwa November 24
KUNDI E
KUNDI F
KUNDI G
KUNDI H
Video za magoli ya FC Barcelona Vs Roma
Video za magoli ya Arsenal Vs Dinamo Zagreb
Video za magoli ya Bayern Munich Vs Olympiakos
Kipigo kilichowakuta AS Roma kwa FC Barcelona bora ya Real Madrid, haya ndio matokeo ya mechi za UEFA Nov 24 (+Video)
Reviewed by habari motto
on
7:05 AM
Rating:
