Kama ni mpenzi wa soka wa muda mrefu huwezi kuacha kumjua David Beckham staa wa zamani wa soka wa Man United, Real Madrid na timu ya taifa ya Uingereza,Beckham ni mchezaji ambaye jezi yake namba saba ilirithiwa na Cristiano Ronaldowakati ambao Beckham alitimkia Real Madrid ya Hispania huku Ronaldo akijiunga naMan United.
Beckham ambaye alikuwa akisifika kwa umahiri wake wa kupiga mipira ya faulo kauli yake imeingia katika headlines baada ya kufunguka katika interview kuwa kama Cristiano Ronaldo atahama Real Madrid ni vizuri akirudi Man United, kauli ambayo inazidi kuongeza uvumi wa staa huyo kuhama Real Madrid ya Hispania.
Beckham
“Sikuwahi kumshauri yoyote kurudi Man United, Cristiano amekuwa kama shabiki wa Man United kwani anaipenda na amefanya vizuri akiwa Old Trafford na kucheza kwa bidii” >>>Beckham
“Kila mmoja ambaye amewahi kucheza na Ronaldo angeongea haya, Ronaldo sio tu ni moja kati ya wachezaji waliokuwa na vipaji vikubwa katika soka bali ni mchezaji anayejituma, binafsi kama ataondoka Real Madrid sehemu sahihi nafikiri anayoweza kwenda ni Man United” >>> Beckham
Ronaldo
Hadi sasa Cristiano Ronaldo ambaye anachezea timu ya taifa ya Ureno na klabu yaReal Madrid amekuwa akihusishwa kuhama Real Madrid na kwenda katika klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, kurudi Man United ya Uingereza au kwenda kucheza soka Marekani mahali ambapo aliripotiwa kununua jumba la kifahari kwa miezi ya hivi karibuni kitu ambacho kinahusishwa na maandalizi ya staa huyo kuhamia Marekani.
Sentensi mbili za David Beckham:kama Cristiano Ronaldo ataondoka Real Madrid
Reviewed by habari motto
on
7:24 AM
Rating: