Chama cha Wananchi CUF kimekanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif ambazo zilianza kusambaa tangu jana jioni kwamba kiongozi huo amefariki dunia
Jussa Ismail Jussa, amesema taarifa hizo sio za kweli. Pia amezungumzia hali ya kisiasa mjini Zanzibar kwamba kwa sasa hali si shwari.
JUSSA: Niwaambie kwamba ni mzima na kwa hakika tuko Dar es Salaam asubuhi na mimi nimefatana nae, asubuhi tumekuja tumekuwa na miadi ya kuonana na balozi wa jamhuri ya watu wa China katika Tanzania. Tumetoka katika mazungumzo hayo, yuko mzima. Jana alikuwa ameendelea na mazungumzo ya vikao ambavyo vinafanyika katika ikulu ya Zanzibar kuhusu suala la mgogoro wa Zanzibar. Hivyo niwatolee wasiwasi, Maalim yuko fiti kabisa. Wapuuze uvumi huu na wawapuuze wenye nia hizi mbaya.
Bahati mbaya kwenye nchi yetu sasa yamekuwa ni mazoea haya, watu wanatumia vibaya mitandao ya kijamii lakini kumekuwa na hii tabia ya kuombeana mabaya tu kila wakatilakini niwaambie njama zao hazitafanikiwa, Maalim Seif anaendelea kufanya kazi zake.
Hali ya kisiasa Zanzibar bado ni ya wasiwasi, mimi nilikuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Malindi na nina cheti changu cha kuthibitisha nimechaguliwa kihalali, watu wengi wanafatilia kwa kina iwapo maamuzi ya ya tarehe 25 Oktoba kama yataheshimiwa.
Hali ya amani itategemea sana kufanikiwa kwa jitihada hizi na nichukue fursa hii kuomba sana viongozi wa Tanzania hasa Rais John Magufuli ambae ameanza kwa kasi nzuri sana asiruhusu suala la Zanzibar kuvuruga kazi nzuri alioifanya na sote kwa pamoja tuchukue jitihada kuona haki inatendeka.
CUF wakanusha taarifa za kifo cha Maalim Seif (VIDEO)
Reviewed by habari motto
on
5:44 PM
Rating: