‘Waliompinduwa’ Nkurunziza Wafugwa Kifungo cha Maisha

Generali Ndayirukiye mmoja wa wanamapinduzi wa Pierre Nkurunziza
Genrali Ndayirukiye mmoja wa wanamapinduzi wa Pierre Nkurunziza
MAHAKAMA nchini Burundi imewahukumu kifungo cha maisha majenerali wa jeshi walioongoza mapinduzi dhidi ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. Mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine tisa miaka 30 jela kwa kitendo cha kuhusika katika jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi.
Wanne kati ya hao watakaotumikia kifungo cha maisha jela ni aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Cyrille Ndayirukiye, Jenerali Zenon Ndabaneze, Juvenal Niyungeko na Hermenegilde Nimenya aliyekuwa Kamishana wa Polisi.
Awali upande wa mashtaka uliiomba mahakama kuwafunga washtakiwa wote kifungo cha maisha baada ya kukiri kushiriki katika jaribio hilo la mapinduzi mnamo mwezi Mei.
BBC
‘Waliompinduwa’ Nkurunziza Wafugwa Kifungo cha Maisha ‘Waliompinduwa’ Nkurunziza Wafugwa Kifungo cha Maisha Reviewed by habari motto on 6:47 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.