Huyu Ndiye Waziri Mkuu Mpya Wa Uingereza

Theresa May
Waziri wa maswala ya ndani wa Uingereza, Theresa May, atatangazwa kinara mpya wa chama cha Conservative, na waziri mkuu mpya wa Uingereza.
Theresa May
Hii ni baada ya mpinzani wake mkuu katika kinyanganyiro ya kuwania kiti cha uaziri mkuu mbunge Andrea Leadsom, kujiondoa.
Uingereza kupata waziri mkuu mwanamke
Andrea Leadsom ameamua kumuunga mkono mpinzani wake, Theresa May kuwania kiti hicho, huku akisema kuwa anatakiwa kutimiza uungwaji wake mkono wa kujiondoa kwa Uingereza kutoka muungano wa jumuia ya mataifa ya EU na kutoa fursa kupatikana kwa haraka kwa waziri mkuu mpya.
Wakuu wa chama cha Conservative kwa sasa wanajadiliana ili kumuidhinisha Bi May, kuchukua nafasi hiyo na kuwa waziri mkuu wa pili wa kike nchini Uingereza baada ya Bi Margaret Thatcher.
Wakati huo huo, Mbunge Angela Eagle ametangaza rasmi nia ya kumn’goa Jeremy Corbyn kama kinara mkuu wa chama cha Leba.
Source: BBC
Huyu Ndiye Waziri Mkuu Mpya Wa Uingereza Huyu Ndiye Waziri Mkuu Mpya Wa Uingereza Reviewed by habari motto on 7:03 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.