Shambulizi linaloaminika kuwa la kigaidi limeua zaidi ya watu 75 wakiwemo watoto huko katika mji wa Nice nchini Ufaransa. Shambulio hilo limetokea kwa mtu kuendesha gari kubwa la mizigo katikati ya watu waliokuwa wamekusanyika kuangalia fataki na kusheherekea sikukuu ya Bastille Day ambayo hulinganishwa na sikukuu ya uhuru nchini Ufaransa.
Vyombo mbalimbali vya habari vinaripoti kwamba gari hilo la mizigo lilikuwa limesheheni silaha na mabomu na kwamba dereva alianza kwanza kuwashambulia watu kwa kutumia silaha kabla ya kuanza kuwakanyaga. Aliendelea kufanya hivyo mpaka alipouawa na polisi kwa kupigwa risasi.
Tayari Rais Hollande amelielezea tukio hilo kuwa la kigaidi na ametangaza kuongeza miezi mitatu katika tangazo la hali ya hatari nchini humo.
Shambulizi La Kigaidi Lateketeza Zaidi Ya Watu 75 Nchini Ufaransa
Reviewed by habari motto
on
6:25 AM
Rating: