Rais Magufuli Amkumbuka Augustine Mrema Na Kumteua Kuwa Mwenyekiti Bodi Ya Parole

Augustine-Mrema-Mwenyekiti-Bodi-Ya Parole
Augustine-Mrema-Mwenyekiti-Bodi-Ya Parole
Ahadi ni deni. Kama utakumbuka wakati wa kampeni za Urais mwaka jana, Rais Magufuli alipofika jimboni Vunjo mkoani Kilimanjaro alikutana na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Augustine Lyatonga Mrema ambaye kwa miaka mingi alihamia kambi ya upinzani.
Mambo yalikuwa hayaendi vizuri kwa Mrema. Nafasi ya ubunge aliyokuwa nayo katika jimbo la Vunjo kupitia chama chake cha TLP ilikuwa hatarini. Kambi ya UKAWA ilikuwa ikitishia kulichukua jimbo la Vunjo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na mgombea wake, James Mbatia.
Mrema aliona mbali. Akatamka wazi kumuunga mkono mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dr. J.P.Magufuli ambaye alikwenda kushinda Urais. Katika mkutano ule wa Vunjo, Mrema alielezea kwamba bado yupo fit na anahitaji “kazi”. Dr.Magufuli alikuwa muungwana na kumwahidi kumfikiria Bw.Augustine Mrema ambaye aliwahi kutamba katika upinzani pengine kushinda wanasiasa wengi wengine.

Yaelekea Dr.Magufuli hakuwa muungwana asiye na nia ya kutimiza ahadi.Kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, akiwemo Bw.Augustine Mrema ambaye amemteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
Mhe. Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.

Pia Dr.Magufuli amefanya teuzi zingine mbalimbali kama zifuatazo;
Prof. William R. Mahalu– Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

Prof. Mohamed Janabi-Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Prof. Angelo Mtitu Mapunda-Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Bi. Sengiro Mulebya-Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Bw. Oliva Joseph Mhaiki-Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa-Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Dkt. Charles Rukiko Majinge-Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.


Dkt. Julius David Mwaiselage-Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Rais Magufuli Amkumbuka Augustine Mrema Na Kumteua Kuwa Mwenyekiti Bodi Ya Parole Rais Magufuli Amkumbuka Augustine Mrema Na Kumteua Kuwa Mwenyekiti Bodi Ya Parole Reviewed by habari motto on 7:39 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.