CAMEROON 1-- 4 BRAZIL

CAMEROON 1-- 4 BRAZIL: NEYMAR APIGA MBILI NA KUFUZU HATUA YA 16 

Nyota: Neymar alifunga magoli mawili dhidi ya  Cameroon katika mchezo wa mwisho wa kundi A.
TIMU ya Taifa ya Brazil imefuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia baada ya kuifunga Cameroon mabao 4-1.
Mshambuliaji hatari,  Neymar alifunga mabao mawili katika dakika ya  17 na 34′,, huku mawili yakifungwa na  Fred katika dakika ya 49 na Fernandinho dakika ya 84′.
Bao la kujifutia machozi kwa Cameroon lilifungwa na Joel Matip katika dakika ya 26 kipindi cha kwanza.
Hata hivyo aina ya mpira wa Brazil wa mwaka 2014 una mapungufu na unaweza kudhani hawatafanikiwa kufika mbali zaidi katika michuano hii.
Lakini Neymar anaoonekana kuipa nguvu zaidi na kubeba michuano hii begani mwake.
Mchezaji mmoja anaweza kuiwezesha timu kutwaa ubingwa?
Labda hapana, lakini Neymar alifanya kazi nzuri katika mchezo huo kuhakikisha timu yake inamaliza vizuri mechi ya mwisho ya makundi.
 Nyota kinda wa Brazil, Neymar akifunga bao la kuongoza katika dakika ya 17

Hapa chini ni vikosi vya timu zote na viwango vya wachezaji. Alama ni chini ya 10.
Kikosi cha Cameroon: Itandje 6; Nyom 5.5, Nkoulou 5.5, Matip 6, Bedimo 5; Mbia 6, Nguemo 6, Enoh 6.5; Choupo Moting 6 (Makoun 80, 5.5), Aboubakar 5.5 (Webo 71, 6), Moukandjo 6 (Salli 57, 5).

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Feudjou, Assou-Ekotto, Djeugoue, Nounkeu, Eto’o, Chedjou, Webo, Fabrice, N’Djock.
Kadi ya njano: Enoh, Mbia

Mfungaji wa goli: Matip 26′
Kikosi cha Brazil: Julio Cesar 6; Alves 6, Silva 6, Luiz 6, Marcelo 5.5; Paulinho 5 (Fernandinho 45, 7.5), Luiz Gustavo 6.5, Oscar 6; Hulk 6 (Ramires 63, 5.5), Neymar 8 (Willian 71, 6); Fred 6.5

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Jefferson, Dante, Maxwell, Henrique, Hernanes, Bernard, Jo, Maicon, Victor.
Wafungaji wa Magoli: Neymar 17, 34‘, Fred 49′, Fernandinho 84′
Idadi ya watazamaji: 69,112
Mchezaji bora wa mechi: Neymar
Mwamuzi:
Jonas Eriksson (Sweden) 6.5
  Neymar alifunga tena bao la pili katika dakika ya 34
 Joel Matip (katikati) akishangilia bao lake la kusawazisha dhidi ya Brazil.


CAMEROON 1-- 4 BRAZIL CAMEROON 1-- 4 BRAZIL Reviewed by habari motto on 9:19 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.