ALSHABAB WAZIDI KUFANYA MAUWAJI, MJI WA PWANI WAVAMIWA

                   Shambulizi la Alshabaab nchini kenya
Kundi la Alshabaab limekiri kutekeleza shambulizi katika basi moja la abiria katika pwani ya Kenya hapo jana usiku.
 Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu saba walipigwa risasi na kufariki huku wengine wengi wakijeruhiwa.
 Shambulizi hilo lilitokea katika mji wa Witu katika Kaunty ya Lamu.
 Watu kadhaa wameuawa katika Pwani ya Kenya katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita.
 Kundi la Alshabaab limekiri kutekeleza mauaji hayo.
 Linasema kuwa linalipiza kisasi kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somali.
Ghasia hizo zimeathiri pakubwa sekta ya utalii nchini Kenya
ALSHABAB WAZIDI KUFANYA MAUWAJI, MJI WA PWANI WAVAMIWA ALSHABAB WAZIDI KUFANYA MAUWAJI, MJI WA PWANI WAVAMIWA Reviewed by habari motto on 5:48 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.