ATHLETICO MADRID YATISHA... YAMNUNUA JAN OBLAK

Mabingwa wa Uhispania Atletico Madrid imekubali dili la kumsainisha mlinda mlango wa Benfica Jan Oblak kwa lengo la kuwa mbadala wa mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois. 
Mlinda mlango wa kimataifa wa Ubelgiji, Courtois, 22, alikuwakwa mkopo wa miaka mitatu na Atletico lakini kutokana na kiwango kizuri alichokionesha msimu uliopita kimemfanya boss wa The Blues Jose Mourinho kukusudia kumrejesha Stamford Bridge.
Mlinda mlango wa Slovenia Oblak amekubali kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka sita. 
Oblak, 21 alitajwa kuwa kipa bora wa Ureno msimu uliopita. 
"Huyu ni kipa mwenye viwango vingi na ambaye atakuwa kwa muda mrefu na kutupatia mafanikio makubwa," amenukuliwa Mkurugenzi wa michezo wa Atletico Jose Luis Caminero.  
Oblak atakuwa na ushindani mkubwa na Miguel Angel Moya, ambaye amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni akitokea Getafe.
ATHLETICO MADRID YATISHA... YAMNUNUA JAN OBLAK ATHLETICO MADRID YATISHA... YAMNUNUA  JAN OBLAK Reviewed by habari motto on 6:50 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.