CRISTIANO
Ronaldo ameshinda tuzo ya Goal 50 ya mchezaji bora wa dunia baada ya kuwa na
msimu mzuri wa 2013-14.
Mshambuliaji
huyo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu kama sehemu ya kuheshimu kazi
aliyoifanyia Real Madrid kutwaa taji la 10 la ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Nyota
huyo mwenye miaka 29, pia alishinda kombe la mfalme (Copa del Rey) na kufunga
magoli 51 katika mashindano yote ya klabu na taifa lake.
WALIOSHINDA TUZO YA Goal 50
mpaka sasa:
2008- Cristiano Ronaldo
2009 -Lionel Messi
2010- Wesley Sneijder
2011-Lionel Messi
2012- Cristiano Ronaldo
2013 -Lionel Messi
2014 -Cristiano Ronaldo.
Ronaldo
alishinda kiatu cha dhahabu sambamba na Luis Suarez na mapema mwaka huu
alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia na kushinda tuzo ya 2013 FIFA Ballon
d`Or.
Baada
ya kupokea tuzo hiyo, Ronaldo alisema: “Ni heshima kubwa kwangu kuchaguliwa
kuwa mchezaji bora. Kiukweli nimefurahi sana”.
“Nashawishika
kusema nisingeweza kutwaa tuzo hii bila sapoti kutoka watu wa Real Madrid”.
Goal
50 ni moja ya tuzo za heshima kwenye mchezo wa soka kwasababu wanaochagua
wanatoka katika mitandao mikubwa ya soka duniani.
Kura
zinapigwa baada ya kumalizika kwa misimu ya ligi za ndani na mashindano ya
kimataifa na wanaopiga kura wanatoka mataifa mbalimbali.
Zaidi
ya waandishi wa habari 600 kutoka katika machapisho 35 wanachagua wachezaji 50
wa juu kwenye tuzo hiyo.
Ronaldo
ameongoza mwaka huu akifuatiwa na Arjen Robben, aliyeifanyia makubwa Uholanzi
katika fainali za kombe la dunia na kuisaidia klabu yake ya Bayern kutwaa
makombe manne msimu wa 2013-14.
Mshindi
wa mwaka jana, Lionel Messi alishika nafasi ya tatu baada ya msimu mbaya katika
klabu yake ya Barcelona na kushindwa kutwaa kombe la dunia nchini Brazil.
CHRISTIANO RONALDO AZIDI KUPAA.. AMBWAGA MESSI KWA KUTWAA TUZO BORA DUNIANI..
Reviewed by habari motto
on
11:19 AM
Rating: