HIKI NDICHOALICHOKISEMA AKON KUHUSU NDOA YA JAY Z NA BEYONCE

beyonce-jayz-blue-ivy-lunch-ftr

Wakati ambapo tetesi za kukaribia kuvunjika kwa ndoa ya Jay Z na Beyonce zikiendelea kushika kasi, msanii mwenzao, Akon amezungumza anachokiona kuhusiana na uhusiano wa mastaa hao



Uhusiano wao umekuwa wa kibiashara katika ulimwengu wa nje kuliko uhusiano wa kawaida,” Akon alimwambia mwandishi wa TMZ aliyemuuliza anauonaje uhusiano wa Jay na Bey. “Ukiwa mtu unayejulikana na una uhusiano, uhusiano wako nao unakuwa wa umma. Hivyo usipofunguka kwa umma, ni kawaida wao kuongea vitu wanavyohisi vinaendelea,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, licha ya fununu za talaka mbele yao, Jumanne hii Beyonce na Jay Z walipiga show ya kufa mtu San Francisco, Calif.
beyonce-jayz-blue-ivy-lunch-ftr
Wanandoa hao walidaiwa kukaa pamoja kwenye hoteli ya kifahari ambayo kwa chumba kimoja (presidential suit) gharama ni $30,000 (zaidi ya shilingi milioni 50) kwa usiku mmoja. Beyonce na Jay Z walikuwa pamoja jioni ya juzi kwenye hoteli ya kifahari St Regis hotel jijini San Francisco, kwa mujibu wa Daily Mail.
StRegis_Astor_Suite_Living_Area
Moja ya sehemu kwenye hoteli hiyo
Wawili hao walikuwa na mtoto Blue Ivy Carter.
HIKI NDICHOALICHOKISEMA AKON KUHUSU NDOA YA JAY Z NA BEYONCE HIKI NDICHOALICHOKISEMA AKON KUHUSU NDOA YA JAY Z NA BEYONCE Reviewed by habari motto on 8:09 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.