NCHI ya Urusi imetoa taarifa kuwa ni marufuku vyakula kutoka kwa muungano wa Ulaya,kuingia nchini huko. Marekani na nchi zingine kadha za magharibi ambazo zilikuwa zimetangaza vikwazo dhidi ya Urusi kutokana na sera zake nchini Ukraine.
Waziri mkuu nchini Urusi Dmitry Medvedev aliuambia mkutano wa serikali kuwa Urusi haitaruhusu tena uingizwaji wa Nyama, Samaki, Matunda na bidhaa zingine kutoka mwa jumuiya ya Ulaya, Marekani, Australia, Canada na Norway.
Medvedev amesema kuwa vikwazo hivyo vitadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Amesema kuwa Urusi inatathmini kupiga marufu mashirika ya ndege ya nchi za magharibi yanayotumia anga ya Urusi kuingia barani Asia.
Wadadisi wanasema kuwa Urusi inategemea zaidi chakula kutoka nje asilimia kubwa ikiwa ni kutoka kwa nchi za magharibi.
NA HII NDIYO TAARIFA YA URUSI,KUHUSU MAHASIMU WAO WA ULAYA..
Reviewed by habari motto
on
2:26 PM
Rating: