Thomas Vermaelen anaelekea kuikera klabu ya Barcelona na meneja wake Arsene Wenger kwa kuchagua kuijunga na Louis van Gaal kwenye klabu ya Manchester United.
Maafisa wa Barcelona wapo jijini London wiki hii katika jaribio lao la kumshawishi mlinzi huyo wa kimatifa wa
Ubelgiji Vermaelen kujiunga nao akitokea Arsenal na wamemuwekea dau kubwa zaidi ya lile alilowekewa na United na wakiahidi kumpa mkataba wa muda mrefu, lakini mlinzi huyo wa kati mwenye umri wa miaka 28 mwenye thamani ya paundi 15million hana mpango wa kwenda Uhispania.

Wenger amekubali nahodha wake huyo kuondoka kwenda kokote lakini hakufurahia ajiunge Old Trafford
Vermaelen anaonekana kuvutiwa na kujiunga na Manchester kwa sababu girlfriend wake ni raia wa England, model Polly Parsons, na wana mtoto wa kiume huku ikidaiwa kwamba ana hamu ya kujiunga na rafiki yake wa zamani Robin van Persie.
Arsenal wako katika maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City ambapo wachezaji watatu wa kimatifa wa Ujerumani Per Mertesacker, Mesut Ozil na Lukas Podolski wakiwa bado kuwasili klabuni hapo lakini ikielezwa kwamba watawasili Jumatatu hii, wakati mlinzi wa Uswis Johan Djourou akikaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Hamburg.
Wakati huo huo mlinzi Bacary Sagna ameungana na wachezaji wa zamani kuhama Emirates kwenda Etihad.
Sagna nafuata nyayo za Kolo Toure, Emmanuel Adebayor, Gael Clichy na Samir Nasri.
Manchester United yakaribia kumnasa mlinzi wa Arsenal Thomas Vermaelen
Reviewed by habari motto
on
11:41 AM
Rating: