YETU macho katika hili; Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi, ambaye juzi jioni alijiunga na Simba kudai kuwa atapambana na Wanajangwani hao kuhakikisha haki yake inapatikana.
Maneno hayo ya Okwi yamekuja baada ya kudai kuwa Yanga imevunja naye mkataba kisha
kumfungulia mashtaka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ya kushindwa
kuzingatia makubaliano yake na klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba wake.
Akizungumza Okwi atahakikisha anapambana Yanga hadi hatua ya mwisho kuhakikisha
anapata haki yake.Alisema klabu yoyote ile inapoingia mkataba na mchezaji inatakiwa
kumlipa fedha zake zote za usajili kwa mujibu wa makubaliano na siyo kumzungusha na
kufanya mambo yake kama viongozi wake wanavyotaka.
“Sina hofu kabisa juu ya jambo hili, naamini haki itapatikana kwa sababu hayo ambayo
Yanga wananipakazia hayana ukweli wowote na kama kuna ukweli basi kutakuwa na
sababu.
Hata hivyo kwa sasa haina haja ya kuongea mambo mengi ila jambo la msingi ambalo
ningependa kusema ni kwamba, nipo tayari kusimama sehemu yoyote ile juu ya jambo
hili ili kuhakikisha haki yangu inapatika.
“Hata kama TFF na Fifa watanihitaji leo hii nitasimama mbele yao na kutoa ushahidi
wangu juu ya jambo hili,” alisema Okwi ambaye Yanga imeachana naye akiwa bado na
mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Yanga ilimsajili Okwi akitokea SC Villa ya Uganda ambayo alijiungana nayo akitokea Etoile
du Sahel ya nchini Tunisia ambayo alikuwa na matatizo nayo.
MANJI AKASIRIKA, ATISHIA KUINUNUA SIMBA YOTE
Reviewed by habari motto
on
12:32 PM
Rating: